Wiki ya utumishi wa Umma imeanza leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambapo ofisi za Serikali na taasisi zake na mashirika yanashiriki katika kuonesha uuma huduma mbalimbali zinazotolewa na ofisi hizo za umma. Pichani juu ni maofisa Habari wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakielekeza watu huduma mbalimbali zinazotelewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Wakala wa Usafiri wa haraka (DART) wameamua kuingia mitini kwakua huenda hata huduma zao ni 0 huko mtaani. Wapo watu wanasema hapa wawaite watu wa Bajaji na Bodaboda au Taxi ndo wake maana ndo waharaka.
Siku ya kwanza ni ngumu kwa baadhi ya mabanda kamaa hili la Shirila la Maendeleo la Taifa (NDC) ambapo niliwakuta maofisa wake tu.
Eneo hili hupokea kero na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, ni banda la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeo ya Makazi, haopa Ofisa wake akielezea namna watu wanavyojenga pasipo kufuata ramani za Mipango miji jambo linalofanya kubomolewa kwa makazi yao.
Bima ya Afya (NHIF) nao wapo katika kuelimisha umma juu ya huduma zao.
Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) nao wapo na vifaa mbalimbali.
Huyu ni Sumu ya Teja, nae yupo katika banda la Taasisi ya Sanaa Bagamoyo ambalo lipo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo.
Haya nayo ni mashirika ya serikali katika sekta ya Habari, niliwakuta Shirika la Mageziti ya Serikali (TSN) lakini TBC bado mambo yalikuwa hayajakaa sawa upande wao.
Idara ya utamaduni nayo ipo na hapa ni ofisa wake akielezea mambo ya Historia na Utamaduni wa mtanzania.
Blogu hii itakuwa ikikuletea matukio mbalimbali ya Wiki ya Utumishi wa Umma kila siku. Tufike katika banda lako piga simu 0755 373999/0717002303.
0 comments:
Post a Comment