Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimeti ya Utumishi wa mma Hab Mkwizu (katikati) akitoa cheti jana mjini Bagamoyo cha kuhitimu mafunzo ya wiki moja kwa watendaji waandamizi wa Serikali jinsi ya kusimamia vizuri miradi ya umma kwa manufaa ya jamii nzima kwa Mkurugenzi msaidizi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Jinsia na Maendeleo ya Jamii Chrizostomu Lushiku.Wengine ni Mkufunzo wa Mafunzo hayo kutoka Uingereza Ralph Naylor(kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo kutoka Ofisi ya Rais Menejimeti ya Utumishi wa Umma Elisante Mbwilo.
Pamoja -Watendaji waandamizi kutoka Idara , Mashirika ya Umma na Wizara mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimeti ya Utumishi wa Umma Hab Mkwizu (wa pili kutoka kulia) jana mjini Bagamoyo mara baada ya kufunga mafunzo ya wiki moja kwa watendaji hao juu ya kusimamia na uendeshaji mzuri wa miradi ya umma kwa manufaa ya wananchi wote.
0 comments:
Post a Comment