KUNDI la muziki wa taarabu la Nadi Ikhwan Safaa kutoka Malindi mjini Zanzibar linataraji kutua jijini Dar es Salaam na kutumbuiza katika ukumbu wa Travertine Ijumaa wiki hii.
Mratibu wa onesho hilo liliandaliwa na Chezntembaa, Abbas Hussein, Cash Money alisema kuwa, kundi hilo likiwa
chini ya mwanamuziki mkongwe Profesa Elias litatoa burudani ya nguvu ya muziki wa asili.
Aliwataja wanamuziki wengine watakaoandamana na kundi hilo ni Fauzia Abdallah, Ally Masoud, Sada Mohamed, Sheria Issa Masoud Mfaume, Bamba, Salum Hamis, Muhamed Issa Matona, na Rukia Ramadhani.
Alisema onesho hilo ni la kuazimisha miaka 106 tangu kuanzishwa kwa kundi hilo kongwe kwa muziki wa taarabu Zanzibar.
Alisema katika onesho hilo kutakuwa na wanamuziki waalikwa ambao watatoa burudani ya kuindikiza Malindi Ikwan Nadia Safaa ambao ni Afua B52, Patricia Hillary na Shakila Said.
Alisema kuwa onesho hilo lilidhaminiwa na Konyagi na Redd's kutakuwa zawadi mbalimbali kwa mashabiki watakaocheza vizuri, kiingilio ni sh.5,000.
Kundi la Nadi Ikhwan Safaa ambalo maana yake halisi ni “Wakaka wanaopendana” lilianzishwa mnamo mwaka 1905 likiwa na wanamusiki wakiume tu na lilikuwa ni kundi la kupiga ala tu. Mwaka 1964 baada ya mapinduzi ya Zanzibar kundi hili lililoanzishwa na Sultan wa Visiwa hivyo lilibadili jina na kuwa Malindi Musical Club.

0 comments:
Post a Comment