Nafasi Ya Matangazo

May 29, 2011

MCHAKATO wa kuendeleza mchezo wa ngumi za Ridhaa Katika MKoa wa Kimichezo wa ILALA, unatarajiwa kuingia katika hatua nyingine Juni 4 kati ya klabu ya ngumi ya Amana na Matimbwa.

Mapambano hayo ya raundi nne, yanatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Panandi  uliopo Ilala Bungoni  jijini Dar es Salaam ambapo mabondia nane kutoka katika kila klabu hizo mbili ikiwa ni wanne kila upande, watachapana masumbwi.

Mabondia wa Amana watakaopanda siku hiyo ni Ibrahimu Class Kg.64,Khalfani Othumani Kg 57, Kassimu Sambo Kg 54, na Saidi Ally Kg 48. Klabu ya Matimbwa itawakilishwa na Mohamedi Matimbwa Kg 64, Mohamedi Muhani Kg 57, Edson Joviki Kg 54 na Mohamedi Kumbilambali Kg 48.

Akizungumza Dar es SAlaam leo Mratibu wa mapambano hayo ambae pia ni kocha wa mchezo wa ngumi akishirikiana na Kinyogoli Foundition, RAjabu Mhamila Super D, Alisema mpango huo utaendelea mpaka wahakikishe wamefanikiwa kuibua vibaji na kuviendeleza.

Alisema tangu waanze mpango wa kuandaa mapambano mkoani humo wamefanikiwa kurudisha hamasa ya mchezo huo na kuwataka wadau mbalimbali kutoa sapoti kwa mchezo huo ili upate kuendelea ambapo Super D alitoa mfano wa vitu wanavyoviitaji ikiwemo posho za nauli kwa wachezaji vifaa vya kuwatia moyo na zawadi mbalimbali kwa mabondia.

Posted by MROKI On Sunday, May 29, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo