Mkurugenzi wa MD Digital Comapny ya jijini Dar es Salaam Mroki Mroki a.k.a Father Kidevu mbali na shughuli ya upigaji picha pia ni mkulima hodari anaetekeleza Mpango wa Kilimo Kwanza kwa vitendo. Pichani ni Mroki akikagua shamba lake la mahindi lililopo kijijini kwake Kinyenze Wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
Mroki akitoa maelezo ya namna ya uwekaji wa dawa ya kuzuia wadudu kwa mtoto wake.
Mroki akielekeza namna ya uwekaji mbolea katika mimea jamii ya mikunde (fiwi nyeusi) alizopanda katika shamba hilo la mahindi.
Hapa akiondoa majani yaliokuwa katikati ya shamba kupisha ukuaji mzuri wa Fiwi.
CDM Thomas Nathan mtaalam kutoka Dynapharm International Dar es Salaam ambao walitoa mbolea maalum ya kupandia na kukuzia aina ya D.I Grower ambayo imekuzia mahindi hayo na kuyafanya yenye kustawi vizuri.




Yaani siku hizi hakunaga NACHURO FUUDS tena!
ReplyDeleteYaani kila kitu kinapewa dawa tu.
Ng'ombe dawa, Kuku dawa, Kitimoto dawa, Mahindi dawa,
Khaah!
Ndo mana siku hizi hatuishi miaka mingi kama wazazi na mababu zetu na pia magonjwa ya ajabu ajabu yamekuwa mengi!
Mweeh!
Heko mkuu!I see unanipa hamasa ya kutafuta shamba nyumbani ili kutekeleza kwa vitendo Kilimo Kwanza...haya masupermarket jamani yanatusahaulisha mambo muhimu na kutufanya tubweteke
ReplyDelete