MISS UTALII TANZANIA KUMSHTAKI LUNDENGA SHIRIKISHO LA DUNIA LA MASHINDANO YA UREMBO, ANYIMWE LESENI YA MISS WORLD MWAKA HUU.
Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo (kushoto)akiwa na warembo wa utalii.
Rais wa Miss Tourism Tanzania Organisation, Erasto Gideon Chipungahelo, ametoa onyo kali kwa Mkurugenzi wa Lino International Agency mwandaaji wa Miss Tanzania Hashimu Lundenga,kuacha mara moja kumfuatafuta yeye na mashindano yao ya Miss Utalii Tanzania, kwa kueneza propaganda za uongo dhidi yake, mashindano ya Miss Utalii Tanzania na kuwarubuni warembo na washindi wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania.
Tumevumilia kwa muda mrefu dhidi ya tabia na mwenendo huo wa Lundenga na mashindano yake wa kueneza propaganda potofu zinazolenga kudhoofisha mashindano ya Miss Utalii na mengine nchini,kwa lengo pia la kuhakikishia kuwa mashindano haya na mengine hayapati udhamini mkubwa hivyo kuzuwia Ustawi na ukuaji wa Sanaa ya urembo nchini.
Huyu bwana Lundenga kila mara wakati wa semina za mawakala wa mashindano yake amekuwa akituongelea vibaya na kutufanya kama sehemu ya ajenda za semina yake,huku akitubeza na kutoa kauli za uongo na kejeli mbele ya mawakala wake,waandishi wa habari na hata wakuu wa makampuni na vipongozi mbalimbali wanao hudhuria semina hizo za mawaka wake.
Mfano halisi ni katika semina ya mawakala wake aliyo ifanya hivi karibuni,ambapo alifukuza waandishi wa habari,ambapo katika moja ya kauli zake alidai eti aliwahi kunifukuza kuwa wakala wake wa mkoa wa Kilimanjaro,jambo ambalo ni uwongo mkubwa na wa aibu, kwani baada ya mwaka 2001 sikuwahi kuomba uwakala kwake baada ya kuwa nilisha anza mchakato wa kuanzisha shindano la Miss Utalii Tanzania,ambalo lilisajiliwa Rasmi mwaka 2002.
Baada ya kuwa Ndani ya shindano hilo la Miss Tanzania kwa zaidi ya miaka miwili na kugundua kuwa shindano hilo haliendani na Utamaduni na maadili ya Kitanzania na mbaya zaidi halina manufaa ya msingi kwa Taifa wala watanzania,niliamua kujitoa mwaka 2001 na kuanzisha Miss Utalii Tanzania,ambalo hadi leo linamnyima usingizi bwana Lundenga na kumfanya aweweseke usiku na mchana akifanya na kutafuta kila mbinu ya kuliua na kulikwamisha kama ambavyo mashindano mengine yalivyo kwama na kufa bila ya mafanikio.
Mfano mwingine hai ni jinsi asivyo zingatia na kuheshimu taratibu na mikataba ya mashindano ya urembo, ambapo Mshindi au washindi wa shindano lolote la urembo nchini na Duniani kwa ujumla haruhusiwi kukubaliwa au kushawishiwa kushiriki au hata kujihusisha na shindano jingine la urembo katika msimu wa ushindi wake,lakini mwaka jana kwa makusudi kabisa na kwa lengo la kuiba na kukopi pateni za Miss Utalii Tanzania ,aliwarubuni washindi wa Miss Utalii Dar es Salaam kwenda kufundisha na kushiriki mashindano yake katika ngazi mbalimbali,wakiwemo Mshindi wa tatu wa Miss Utalii Dar Es Salaam,Mariam Hamisi,Mshindi wa nne Agatha Kilala na Mshindi wa tano Shymaa Mtetema.
Kama haitoshi akiwa na akili timamu huku akijua kabisa ni kosa na ni kinyume cha taratibu,alimrubuni Mshindi wa pili wa Miss Utalii Tanzania 2011,Happywhitney Andrew kwenda kufundisha Miss Tabata 2011,pale Dar West Park. Lakini huko nyuma alimrubuni Mshindi wetu wa Dunia wa taji la Miss Tourism World Bikini 2007-Africa,Ritha Kavishe kiasi cha kumfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake kuliko pelekea uongozi wa Taifa na Dunia kumwengua,katika shughuli zote za kitaifa na kimataifa.
Haya ni machache kati ya mengi,ambayo yeye na kikosi kazi chake cha propaganda kongwe na zisizofaa dhidi ya mashindano mengine amekuwa akizifanya kila mara anapo pata fulsa ya kukutana na wadau,makampuni na hata viongozi mbalimbali.
"Tumevumilia sana,sasa tumechoka huu ni kama aina ya ufisadi ambao kwa hakika ukiachwa kuendelea utaua Sanaa ya urembo nchini,na kuharibu kabisa jina zuri na picha ya Tanzania ambayo Miss Utalii Tanzania tumeijenga kimataifa kupitia mafanikio na mapinduzi makubwa katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.Tunaamini,na kjumshauri bwana Lundenga aondokane na fikra kongwe na za kikiritimba za kutaka kuhodhi Sanaa ya urembo na kuchukulia kila shindano linaloanzishwa na kuwa na mafanikio kama adui".
Dunia ya sasa ni ya kuungana na kushirikiana na sikuhujumiana.Maslahi ya Taifa Kwanza kwa Faida ya kizazi cha sasa na cha badae na siubinafsi na kukusa uzalendo. Sanaa ya urembo inanguvu na uwezo mkubwa wa kuchangia kukuza uchumi na pato la taifa kitaifa na kimataifa,kama tutaungana na kuweka mbele maslahi ya Taifa.
Kwetu sisi,Miss Tanzania imeporomoka na kupoteza kabisa mwelekeo na maudhui ya shindano hilo na hata la Miss World,Lundenga asitafute mchawi ila aka echini na kamati yake waangalie namna na mbinu ya kurudi kwenye msitari kwa kuzingatia Malengo na misingi ya kuanzishwa kwa Miss World ambayo Miss Tanzania ni kopi yake,na sio kuwaota akina Chipungahelo na Miss Utalii Tanzania usiku na mchana.
Baada ya kuwa tumefikisha malalamiko yetu kwa Mamlaka Husika nchini,juu ya mchezo huu mchafu wa Lundenga na Miss Tanzania yake dhidi ya mashindano na waandaaji wa mashindano mengine,na yeye kuto acha tabia na mchezo huo, sasa tunatoa onyo la mwisho kwake aula tutafikisha malalamiko yetu katika World Beauty Pageant Association,ili hatua za kufaa kimataifa zichukuliwe dhidi yake.
Tunamkumbusha bwana Lundenga kuwa,tunao uwezo wa kuchukua leseni ya Miss World,kwani leseni hiyo iko wazi kwa mtu au kampuni yoyote nchini kila mwaka. Leseni ya kupeleka mrembo Miss World inaombwa kila mwaka na hutolewa kwa msimu wa mwaka mmoja,ambapo hata yeye hiulazimika kuomba kila mwaka,hivyo iwapo mtu yeyete akiomba na kuwaridhisha waandaaji wa Miss world wanaweza kumpa na si lazima yeye.
Lakini hatulazimiki kufanya hivyo,iwapo atajirekebisha na kutambua kuwa kila mmoja anayo haki ya kuendesha mashindano ya urembo nchini bila ya kuingiliwa wala kufanyiwa propaganda mbaya na mwingine,ili mradi tu anafuata sheria na taratibu za nchi.Wakati sasa umefika ,tena wakati sahihi kwa wadau na waandaaji wote wa mashindano ya urembo kubadilika na kuunganisha nguvu pamoja kujenga, kuinua na kuendeleza Sanaa ya urembo nchini na si kupigana vita ,majungu na fitina.
Miss Utalii Tanzania ni alama ya Urithi wa taifa –Utalii ni Maisha, Utamaduni ni Uhai wa Taifa.
Asante,
Erasto .G.Chipungahelo
Rais Miss Tourism Tanzania Organisation
0 comments:
Post a Comment