Nafasi Ya Matangazo

July 01, 2010

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi (kulia)akimkabidhi kikombe cha Ushindi wa jumla wa Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2010, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC), Simon Matta, ambayo ilitolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ambapo TCC ilishinda tuzo 6 ikiwemo ya jumla.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wao, Simon Matta,(katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na tuzo zao mbalimbali walizo shinda ikiwa ni pamoja na tuzo ya Jumla ya Mwajiri Bora wa Mwaka walizokabidhiwa jana Dar es Salaam. Wengine walioshika tuzo hizo ni kutoka kushoto ni Training and Development Manager Vitor Kimario, Brand Manager Tunu Kinabo, Human Resources Director Caroline Kavishe, Communications Manager Sara Majengo na Human Resource Business Partner arindwa Shaidi.
CEO wa TCC Simon Matta akiwa katika tafakuri juu ya ushindi walioupata.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) Simon Matta akionesha tuzo ya Mwajiri bora wa Mwaka aliyokabidhiwa juzi na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) muda mfupi baada ya kuipokea kutoka kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi(hayupo pichani). TCC pamoja na tuzo ya jumla ilishinda tuzo nyingine 5 za vigezo tofauti. Wafanyakazi wa Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) wakifurahia tuzo sita walizopata kutoka kwa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ikiwemo ya mwajiri Bora wa Mwaka mara baada ya kukabidhiwa Dar es Salaam juzi. Wa tatu kushoto ni Afisa Mtendaji mkuu, Simon Matta.
Baadhi ya wafanyakazi wa TCC waliohudhuria hafla hiyo wakishangilia pindi walipotajwa kuwa washindi.
Pamela Atengo (katikati) na Mkurugenzi Rasimali watu wa TCC, Caroline Kavishe wakipokea tuzo ya Mahusiano ya Wafanyakazi kutoka kwa Mwakilishi kutoka Kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom.
Narindwa Shaidi akipokea tuzo ya Usawa wa Jinsia kutoka kwa CEO wa Phoenix Issuarance SC Wadhawan.

Posted by MROKI On Thursday, July 01, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo