Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel Bw. Noel Heritty akimkabidhi kapteni wa Mwamko FC zawadi ya Tsh 300,000 baada ya kuibuka mshindi wa kwanza jana baada ya kuifunga timu ya Zantel FC kwa mabao 3 – 2 yaliyopatikana kwa njia ya penati katika bonanza la Dondoka Sauz liliondaliwa na Zantel jana katika viwanja vya shule ya msingi ya Madenge Temeke. Mwamko FC waliondoka na Tsh 500,000 baada ya timu ya Zantel iliyoshike nafasi ya pili kuipa Mwamko FC zawadi yake ya Tsh 200,000 ikiwa ni ishara ya kuunga mkono jitihada za Mwamko FC kuendeleza soka Temeke.
Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel Bw. Noel Heritty akimkabidhi kapteni wa Zantel FC Najim Soud Ali zawadi ya Tsh 200,000 baada ya kuibuka mshindi wa pili katika bonanza la Dondoka Sauz lililoandaliwa na Zantel jana katika viwanja vya shule ya msingi ya Madenge Temeke. Hata hivyo timu ya Zantel ilirudisha zawadi hiyo na kuipatia timu ya MWAMKO FC kama ishara ya kuunga mkono maendeleo ya soka ya timu ya Mwamko FC.
0 comments:
Post a Comment