Nafasi Ya Matangazo

April 29, 2015

Wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga, wakimshangilia Meneja Mkee wa mgodi huo, baada ya kumpatia zawadi ya Meneja bora wa mwaka ambaye wao wenyewe wafanyakazi walimteua. Katika hatua  nyinghine, kampuni ya Acacia imewazawadia saruji na mabati wafanyakazi wake 510 wanaofanyakazi kwenye mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu 500 kwa kuhudumu kwa muda mrefu na 10 kwa kufanya kazi kwa kuzingatia sera mpya ya kampuni hiyo ya tabia sita (Six Desired Behaviors). Utoaji wa zawadi hizo ulifanyika wakati wa sherehe za siku ya wafanyakazi duniani kwa wafanyakazi wa mgodi huo, Jumanne usiku Aprili 28, 2015. Sherehe za Mei Mosi zitafanyika kitaifa mkoani Mwanza
Michell akipongezwa na baadhi ya wafanyakazi
Michell akimtunuku cheti mmoja wa wafanyakazi waliohudumu kwa muda mrefu kwenye mgodi huo,  Joyce Mgaya
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa kwenye maandamano ya kusherehekea sikukuu hiyo hapo mgodini
Michell akiwa katikan picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi waliofanyakazi kwenye mgodi huo kwa muda mrefu
Mtaalamu wa ukuzaji biashara wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, Justine McDonald, (kushoto), akimtunuku cheti cha utambuzi, mmoja wa wafanyakazi 10 bora mwaka huu, Joseph Ngowi.
PICHA ZAIDI BOFYA>>>>>FK MATUKIO
Posted by MROKI On Wednesday, April 29, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo