Naibu Meya wa Jiji la Arusha Prosper Msofe akiwa na watangazaji wa
Redio 5 arusha,wa kwanza kushoto Hilda Kinabo,Mwangaza Jumanne na Akida
Kilango wakifuatilia mashindano ya ndondo Cup yaliyoandaliwa na kampuni
ya Tan Communication Media ya jijini Arusha.
Wachezaji wa timu ya Umbrella Garden wakielekea katika lango kupiga mikwaju ya Penalti mara baada ya kutoka sare ya goli 1-1
mchezaji wa Nyota Fc akipiga Penelti katika lango la Umbrela Garden
Mashabiki wa Nyota Fc wakishangilia Ushindi mara baada ya timu yao kuinyuka Umbrella garden magoli 6-5
********
Timu ya Soka ya Nyota
Fc imeichapa timu ya Ambrella Garden
Fc kwa
Magoli Sita kwa Matano na kufanikiwa
kuondoka na kombe la Ndondo Cup Sambamba
na Kitita cha Shilingi Laki Tano Taslimu
katika fainali za Ndondo Cup zilizofanyika katika viwanja vya Aicc
vilivyopo Jijini Arusha.
Akizungumza wakati wa fainali hizo Naibu meya wa Jiji la
Arusha Prosper Msofe alisema kuwa mashindano hayo ya ndondo Cup yamewakutananisha vijana wengi ambao wamepata
fursa ya kuonesha vipaji vyao.
Prosper Msofe alisema kuwa mkoa wa Arusha una sifa nyingi
lakini katika upande wa Soka kwa sasa Hakuna timu ambayo ipo imara ambao inafanya vizuri katika ligi mbali mbali hapa
nchini.
Aidha Msofe alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa wanaibua
vipaji zaidi na kutengeneza timu moja ya mkoa Jiji la Arusha limepanga kununua
eneo la kiwanja nje ya mji na kutengeneza uwanja bora wa kisasa ambao
utawawezesha vijana wanaopenda kandanda mkoani Arusha kupata sehemu za kuonesha
vipaji vyao na badae kuchuja vijana 20 ambao wataunda timu moja ambayo
itawakilisha mkoa wa Arusha katika mashindano mbalimbali hapa nchini.
Kwa sasa hatuna maeneo ya wazi na hili ni changamoto kwetu
vijana wetu wana vipaji lakini hawana sehemu ya konesha tumepanga kununua
viwanja na kuvitengeneza ili tuanzishe mashindano mbalimbali ambayo yatapelekea
tuapte timu bora itakayotuwakilisha vizuri mkoa wetu wa arusha alisema Msofe
Kwa upande wake waandaaji wa
Ndondo Cup ambayo ni kampuni ya Tan Communication Media Mathew Philip
alisema kuwa lengo la mashindano hayo ya ni kutoa burudani ya soka la Mchangani
kwa wakazi wa Jiji la Arusha lakini pia kuwapa vijana nafasi ya kuonesha vipaji
vyao katika mchezo wa soka.
Mathew alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kutoa burdani
mbali mbali kwa wakazi wa Jiji la Arusha huku akisema kuwa mkoa wa Arusha kwa muda mrefu hakukuwa na Soka la Mchangani
ambalo lina vijana wengi ambao wana vipaji na kuwawezesha kuonesha uwezo wao
kwa kuwa sasa mpira ni Ajira.
Timu zilizoshiriki ni Pamoja na Nyota Fc ambao waliibuka
washindi,Ambrella Garden ambao walishika nafasi ya Pili na kujinyakulia
shilingi laki tatu,F.F.U Oljoro Fc,Njiro
Sports,Tanzanite Fc,Red Star Fc,Lemara Boys,
0 comments:
Post a Comment