Wafanyakazi
wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala mkoani
Shinyanga, wakimshangilia Meneja Mkee wa mgodi huo, baada ya kumpatia
zawadi ya Meneja bora wa mwaka ambaye wao wenyewe wafanyakazi walimteua.
Katika hatua nyinghine, kampuni ya Acacia imewazawadia saruji na
mabati wafanyakazi wake 510 wanaofanyakazi kwenye mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu 500 kwa kuhudumu kwa muda mrefu na 10 kwa kufanya kazi kwa
kuzingatia sera mpya ya kampuni hiyo ya tabia sita (Six Desired
Behaviors). Utoaji wa zawadi hizo ulifanyika wakati wa sherehe za siku
ya wafanyakazi duniani kwa wafanyakazi wa mgodi huo, Jumanne usiku
Aprili 28, 2015. Sherehe za Mei Mosi zitafanyika kitaifa mkoani Mwanza
Michell akipongezwa na baadhi ya wafanyakazi
Michell akimtunuku cheti mmoja wa wafanyakazi waliohudumu kwa muda mrefu kwenye mgodi huo, Joyce Mgaya
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa kwenye maandamano ya kusherehekea sikukuu hiyo hapo mgodini
Michell akiwa katikan picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi waliofanyakazi kwenye mgodi huo kwa muda mrefu
Mtaalamu
wa ukuzaji biashara wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, Justine
McDonald, (kushoto), akimtunuku cheti cha utambuzi, mmoja wa wafanyakazi
10 bora mwaka huu, Joseph Ngowi.
PICHA ZAIDI BOFYA>>>>>FK MATUKIO
0 comments:
Post a Comment