Nafasi Ya Matangazo

August 20, 2026





Na Mwandishi Wetu, Tanga.
Ajali ya moto iliyotokea usiku wa Agosti 14, 2026, Barabara ya 12, Jijini Tanga, ambayo iliteketeza maduka 12 ya wafanyabiashara, imewaibua Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani humo, ambapo wamefika eneo la ajali na kuwapa mkono wa pole wafanyabiashara hao.

Akizungumzia suala hilo, Agosti 18, 2026, Meneja TRA mkoa wa Tanga, CPA Castro John, amesema wameguswa na tukio hilo la moto kwani wafanyabiashara ni wadau muhimu katika ulipaji kodi nchini.

"Wafanyabiashara wameunguliwa karibu vitu vyao vyote, tumekuja kuwapa pole na kuonyesha mshikamano, pia tumekuja kuwapa kiasi cha fedha kidogo kama kianzio kutokana na wengi wao kupoteza mali zao zote," amesema CPA John.

Ameongeza kuwa, TRA inawajibika si tu kukusanya kodi lakini pia kuwalea wafanyabiashara waweze kustawi na kukua kibiashara, hivyo, wanapopata majanga ya aina hiyo, wanalo jukumu la kuwashika mkono.

"TRA ina jukumu la kukusanya kodi lakini pia kuhakikisha wafanyabiashara wanastawi. Tutawaita waje ofisini tuongee nao na kuona tunawasaidiaje ili wapate unafuu wa kodi," amesema.

Katika hatua nyingine, Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani humo, Ismail Masoud, amempongeza Meneje TRA mkoa na Kamishna Mkuu kwa kuthibitisha kwa vitendo kuwa wafanyabiashara ni familia moja na TRA.

Pia, ameatoa wito kwa wafanyabiashara wote wa Mkoa wa Tanga kuendelea kulipa kodi kwani kodi hizo ndizo zimesaidia hata kupata misaada hiyo.

Kwa upande wa wafanyabiashara hao, wameushukuru uongozi wa TRA kwa kuwafariji na kuwapa mkono wa pole kwani wapo katika kipindi kigumu kutokana na wengi wao kupoteza mali zao zote.
Posted by MROKI On Thursday, August 20, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo