Nafasi Ya Matangazo

April 11, 2026

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu), Dkt. James Henry Kilabuko (wapili kulia) akishiriki kuimba Wimbo wa Wafanyakazi wakati wa ufunguzi wa Barala la Wafanyakazi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi lililokutana leo Aprili 11, 2026 mkoani Morogoro. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Baraza hilo na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Ramadhani Kailima (wapili kushoto), Katibu wa Baraza, Livini Avith (kulia) na Kulia ni mtumishi wa Tume, Rose Tengu. 
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wakishiriki kuimba Wimbo wa Wafanyakazi wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Barala la Wafanyakazi  INEC lililokutana leo Aprili 11, 2026 mkoani Morogoro. 
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu), Dkt. James Henry Kilabuko akizungumza wakati wa kufungua baraza la Wafanyakazi la INEC. 
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi INEC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhani Kailima akizungumza katika kikao hicho cha Baraza. 
****************
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Watumishi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia katiba, sheria, kanuni  na taratibu na kuepuka lugha zozote za uchochezi zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani na kuhatarisha maisha ya Watanzania.
 
Hayo yamesemwa leo Aprili 11, 2026 na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu), Dkt. James Henry Kilabuko kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt Jimmy Yonaz wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, katika kikao kilichoketi Mkoani Morogoro.
 
“Napenda kuwaasa, kuzingatia katiba, sheria, kanuni  na taratibu mnapotekeleza majukumu ya Tume na kuepuka lugha zozote za uchochezi zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani na kuhatarisha maisha ya Watanzania,”alisema Dkt Kilabuko.
 
Dkt. Kilabuko amesema, taasisi ina malengo yake, upo uwezakano wa kuepusha migogoro ya ndani na nje ya taasisi inayoweza kuathiri utekelezaji wa majukumu ya Tume kwa ufanisi.
  
Mapema akimkaribisha Mgeni Rasmi, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi INEC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhani Kailima alisema kwa sasa Tume inaendelea na zoezi la uandishi wa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2025.
 
“Tume imekamilisha Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ambao ulifanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.  Kwa sasa Tume inaendelea na zoezi la uandishi wa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2025. Taarifa hiyo baada ya kukamilika, itawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”alisema Kailima.
 
Aidha, amesema Tume ipo katika maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Isimani mkoani Iringa kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe. William Lukuvi pamoja na uchaguzi wa udiwani katika Kata mbalimbali nchini ambazo madiwani wake walifariki.
 
Katika Kikao hicho cha siku moja pia kilitumika kwa kufanya uchaguzi wa Katibu wa Baraza hilo ambapo wajumbe walimchagua Ndg. Mwitaru Keboya kuwa Katibu mpya wa Baraza akichukua nafasi ya Ndg. Livini Avith ambaye amemaliza muda wake.
Katibu Mpya wa baraza la Wafanyakazi INEC, Ndg. Mwitaru Keboya akizungumza. 
Katibu wa Baraza aliyemaliza muda wake, Ndg. Livini Avith akizungumza. 

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi INEC wakifuatilia agenda mbalimbali katika mkutano huo. 

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi INEC wakifuatilia agenda mbalimbali katika mkutano huo. 

Mwenyekiti wa TUGHE tawi la INEC, Ndg. Juvenile Kaiza akizungumza.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi INEC wakifuatilia agenda mbalimbali katika mkutano huo. 
Posted by MROKI On Saturday, April 11, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo