Nafasi Ya Matangazo

February 06, 2026



Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana,  imesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Benki ya CRDB kupitia CRDB Bank Foundation kwa ajili ya uendeshaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, hatua inayolenga kuimarisha uwezeshaji wa vijana kiuchumi, kijamii na kitaaluma nchini.

Hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo imefanyika katika Ofisi za Wizara ya Maendeleo ya Vijana zilizopo Mtumba, jijini Dodoma, na kushuhudiwa na Mheshimiwa Joel Arthur Nanauka, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana.

Katika hatua muhimu ya utekelezaji wa mfuko huo, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameidhinisha na kutoa jumla ya Shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kuanza rasmi kwa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Fedha hizo zinalenga kuwawezesha vijana kunufaika na fursa za mikopo nafuu, ujasiriamali, ubunifu, ajira pamoja na miradi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Hundi ya fedha hizo imekabidhiwa rasmi na Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mheshimiwa Joel Arthur Nanauka, katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi za Waziri Mkuu, Mji wa Serikali, jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Vijana amesema kuwa kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ni uthibitisho wa dhamira thabiti ya Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais, ya kuwawezesha vijana kiuchumi, kuwaandaa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa, na kujenga msingi imara wa kizazi chenye tija kwa sasa na baadaye


Posted by MROKI On Friday, February 06, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo