Nafasi Ya Matangazo

February 06, 2026

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara akizungumza na wananachi na wanachama wa CCM Wilaya Bunda leo februari 05 katika Sherehe za Maazimisho ya  Miaka 49 ya Kuzaliwa kwa CCM, Mkoani Mara katika Viwanja Vya Stendi ya Zamani
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara akizungumza na wananachi na wanachama wa CCM Wilaya Bunda leo februari 05 katika Sherehe za Maazimisho ya  Miaka 49 ya Kuzaliwa kwa CCM, Mkoani Mara katika Viwanja Vya Stendi ya Zamani.
***************
Na Mwandishi Wetu, Bunda
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesisitiza umoja wa wanachama ndiyo uliokiwezesha Chama kufanya mambo makubwa.

Wasira alisema hayo leo mjini Bunda katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa CCM.

“Niwaambie kwamba umoja ni nguvu na msingi wa CCM, hakuna CCM kama hakuna umoja, nguvu yetu ni wanachama wetu wa CCM na wanachama hao nguvu yao ni umoja wao, na umoja huo ndiyo umetufikisha hapa, kwa muda mfupi wa siku nane tumechangisha sh. milioni 400,” alisema.

Aidha, Wasira alisema kwa miaka 49 Chama kimefanikiwa kubaki imara na kukubalika kwa wananchi kwa kinasikiliza mahitaji ya Watanzania.

“Mwaka 1962 baada ya kujitawala Mwalimu Julius Nyerere alilitangazia taifa kwamba kuna maadui watatu ambao tunatakiwa kupambana nao (ujinga, maradhi na umaskini), kauli hiyo ilichukuliwa na TANU na kauli hiyo inatekelezwa CCM,” alisema na kusisitiza kuwa, huo ni msingi wa Chama kuwahudumia wananchi wakati wote.

Katika mkutano huo, Wasira aliongoza uchangiaji wa kufanikisha ujenzi wa ofisi ya CCM ya wilaya ya Bunda Mkoa wa Mara na kufanikisha kupatikana zaidi ya sh milioni 400. 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara akikagua athari za uharibifu wa Ofisi ya CCM Wilaya Bunda leo februari 05 akita wilayani humo kwa ajili ya Maazimisho ya Cherche za Miaka 49 ya Kuzaliwa kwa CCM.
Posted by MROKI On Friday, February 06, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo