Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amewakabidhi wananchi watatu Hatimiliki za Ardhi wakati wa hafla ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.
Baada ya kutembelea banda la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Waziri Simbachawene ameipongeza Wizara hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya na kusisitiza kuzuia migogoro inayoweza kutokea kwa kudhibiti vishoka ambao wanaharibu sekta ya Ardhi.
Katika hatua nyingine Simbachawene amesema ushirikiano katika utoaji wa huduma za ardhi lazima uimarishwe kwa sababu Menejimenti ya Wizara ya Ardhi inaanzia chini ambako wananishi watu.
"Ardhi haiwezi ikamilikishwa kama kuna migogoro" amesema Waziri Simbachawene.
Wananchi ambao wamekabidhiwa hati na Waziri Simbachawene ni pamoja na Audax Albert Mbelwa, Elisa Mbise na Godwin Ngele.
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yamefunguliwa Juni 17, 2025 na Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene na yatahitimishwa Juni 23, 2025.
0 comments:
Post a Comment