Uchaguzi wa nafasi tatu za uwakilishi katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) umefanyika leo Mei 4, 2026 Bungeni jijini Dodoma.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamewachagua wagombea watatu kuwa Wabunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) katika uchaguzi
uliofanyika leo Mei 04, 2026 wa kujaza nafasi tatu za Wabunge wa EALA.
Katika Uchaguzi huo wabunge 293 walishiriki kupiga kura hizo za ndio na NDIO na HAPANA na waliwachagua
Fatma Kange, Cosato Chumi na Kambarage Wasira kuwa wabunge wa EALA.
Ndugu Kange alipata kura za NDIO 223 sawa na asilimia 76.1
huku kura za HAPANA zikiwa 70.
Aidha wabunge 289 Sawa na asilimia 98.6 walimpa kura za
NDIOndugu Cosato Chumi na kura nne zikisema HAPANA hivyo kutangazwa kuwa Mbunge
wa Bunge la Afrika Mashariki.
Mtoto wa Mwanasiasa mkongwe wa Tanzania Steven Wasira Ndugu Kambarage
Wasira alichaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki kwa
kupata kura za NDIO 284 sawa na asilimia 96.9 huku kura tisa zikimkataa kwa
HAPANA.
Bunge la Tanzania limetangaza kuwa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi tatu za uwakilishi katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) utafanyika Mei 4, 2026. Hatua hiyo inakuja kufuatia nafasi zilizoachwa wazi baada ya baadhi ya wabunge wa EALA kuchaguliwa kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.










0 comments:
Post a Comment