Nafasi Ya Matangazo

February 18, 2025

Mkuu wa Mkoa ya Manyara, Mhe.Queen Sendiga,akizungumza leo Februari 18,2025 wakati akifungua Mafunzo ya Usimamizi wa Vyama vya Ushirika kwa Maafisa Ushirika wa Kanda ya Kaskazini mjini Babati - Manyara ambayo yataendelea mpaka tarehe 28/02/2025 ambayo yamejumuisha Maafisa Ushirika 116.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Ushirika na Umwagiliaji, Dkt. Stephen Nindi,akizungumza wakati wa Mafunzo ya Usimamizi wa Vyama vya Ushirika kwa Maafisa Ushirika wa Kanda ya Kaskazini mjini Babati - Manyara ambayo yataendelea mpaka tarehe 28/02/2025 ambayo yamejumuisha Maafisa Ushirika 116.
Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Bi.Maryan Muhaji,akizungumza wakati wa Mafunzo ya Usimamizi wa Vyama vya Ushirika kwa Maafisa Ushirika wa Kanda ya Kaskazini mjini Babati - Manyara ambayo yataendelea mpaka tarehe 28/02/2025 ambayo yamejumuisha Maafisa Ushirika 116.
Mrajis na Mtendaji Mkuu Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege,akizungumza wakati wa Mafunzo ya Usimamizi wa Vyama vya Ushirika kwa Maafisa Ushirika wa Kanda ya Kaskazini mjini Babati - Manyara ambayo yataendelea mpaka tarehe 28/02/2025 ambayo yamejumuisha Maafisa Ushirika 116.
Naibu Mrajis Udhibiti Bw.Collins Nyakunga,akizungumza wakati wa Mafunzo ya Usimamizi wa Vyama vya Ushirika kwa Maafisa Ushirika wa Kanda ya Kaskazini mjini Babati - Manyara ambayo yataendelea mpaka tarehe 28/02/2025 ambayo yamejumuisha Maafisa Ushirika 116.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu CPA Jeremiah Mugeta,akizungumza wakati wa Mafunzo ya Usimamizi wa Vyama vya Ushirika kwa Maafisa Ushirika wa Kanda ya Kaskazini mjini Babati - Manyara ambayo yataendelea mpaka tarehe 28/02/2025 ambayo yamejumuisha Maafisa Ushirika 116.
Sehemu ya washiriki wasikiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa ya Manyara, Mhe. Queen Sendiga (hayupo pichani) wakati akifungua Mafunzo ya Usimamizi wa Vyama vya Ushirika kwa Maafisa Ushirika wa Kanda ya Kaskazini mjini Babati - Manyara ambayo yataendelea mpaka tarehe 28/02/2025 ambayo yamejumuisha Maafisa Ushirika 116.

Mkuu wa Mkoa ya Manyara, Mhe. Queen Sendiga,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mafunzo ya Usimamizi wa Vyama vya Ushirika kwa Maafisa Ushirika wa Kanda ya Kaskazini mjini Babati - Manyara ambayo yataendelea mpaka tarehe 28/02/2025 ambayo yamejumuisha Maafisa Ushirika 116.

*********************
Mkuu wa Mkoa ya Manyara, Mhe. Queen Sendiga ametoa rai kwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kufanya mafunzo kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika kama ambavyo wanapatiwa mafunzo Maafisa Ushirika.

Amesema Maafisa Ushirika wanaopatiwa mafunzo wakirudi kwenye Vyama vya Ushirika wanavyovisimamia watakuwa na morali ya kubadili yale ambayo walikuwa wanayafanya bila kufuata utaratibu, ila watakosa ushirikiano kutoka kwa Viongozi wa Vyama kwasababu wao hawajapata Mafunzo hayo.

Ameeleza hayo, leo tarehe 18/02/2025 wakati wa kufungua Mafunzo ya Usimamizi wa Vyama vya Ushirika kwa Maafisa Ushirika wa Kanda ya Kaskazini mjini Babati - Manyara ambayo yataendelea mpaka tarehe 28/02/2025 ambayo yamejumuisha Maafisa Ushirika 116.

“Kumekuwa na tabia ya viongozi wa Vyama kujisahau na kuona kama vile Vyama ni mali zao binafsi na kusahau kuwa chama ni mali ya mwanachama na wanapaswa ufanye kazi kwa malengo ya Chama na si yako binafsi,” amesema Sendiga.

Ameeleza kuwa, Vyama vya Ushirika ili vifike mbali, Maadili na nidhamu ya pesa inahitajika kwa Viongozi na Maafisa Ushirika kwani vikikosekana hivyo vitu viwili hakuna Chama cha Ushirika kinaweza kupata mafanikio au kwa namna yoyote ile.

Pia ameelezea Matumizi ya TEHAMA ndiyo muelekeo wa Serikali katika kila kitu na hivyo ni muhimu Maafisa Ushirika watumie Mfumo wa MUVU katika Utendaji kazi wao hali itakayorahisisha hadi upatikanaji wa taarifa

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Ushirika na Umwagiliaji, Dkt. Stephen Nindi, amesema ni matarajio ya Serikali kwamba mafunzo haya yatawajengea uwezo na kuwafanya Maafisa Ushirika kufanya kazi zao kwa umahiri na weledi ambao utaongeza ufanisi katika Vyama vya Ushirika na kupunguza kwa kiasi kikubwa kasoro mbalimbali zinazojitokeza ikiwa ni pamoja na kupunguza idadi ya Hati za ukaguzi zisizoridhisha kwa Vyama vya Ushirika.

Kwa Upande wake Mrajis na Mtendaji Mkuu Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege, amesema Maafisa Ushirika wanaopata Mafunzo haya wanatakiwa kuzingatia na kuyafanyia kazi Mafunzo wanayopewa wakirudi katika maeneo yao ya kiutumishi.

Posted by MROKI On Tuesday, February 18, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo