Nafasi Ya Matangazo

February 16, 2025






Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ameipongeza Wizara ya Nishati kwa usimamizi wa mradi wa kimkakati wa kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere utakaozalisha Mw 2115 na hivyo kuleta ziada ya upatikanaji wa Umeme hapa nchini.

Msigwa ametoa pongezi hizo leo Februari 16, 2025 katika eneo la mradi wa Julius Nyerere katika Mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali na Waandishi wa Habari wenye lengo la kuzungumzia mafanikio kwenye sekta ya nishati sambamba na maendeleo ya mradi wa kufua Umeme wa JNHPP.

"Wizara hii  kupitia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati Mhe. Dkt Doto Biteko,inafanya kazi kubwa ya kutekeleza mradi huu na mingine ambayo inawanufaisha watanzania kwa kuwapatia umeme wa kutosha." Amesema Msigwa.

Amesema mradi wa bwawa la Julius Nyerere unahusisha mambo makubwa matatu ambayo ni upatikanaji wa  umeme, kilimo kwenye umwagiliaji pamoja na uvuvi kwenye ufugaji na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa zilizopo  kwa maslahi mapana ya nchi.

Aidha, mradi ulianza kujengwa mwaka 2019 kwa gharama ya shilingi trillioni 6.558 ambapo hadi sasa umefikia asilimia 99.8 na mashine nane Kati ya Tisa zimesha kamilika ambazo zimeingiza kwenye gridi ya Taifa megawati kwa jumla ya megawati 1,880.

Msigwa amesisitiza kuwa mashine ya mwisho namba tisa utekelezaji wake umefika asilimia 98 huku majaribio ya mtambo huo yakitarajiwa kuanza majaribio Februari 25 na Machi 10 utaingiza umeme kwenye gridi ya Taifa ili kukamilisha megawati 2,115.

Katika hatua nyingine ametoa rai kwa Watanzania  kujivunia mradi wa Julius Nyerere kutokana na ukubwa wake si katika bara la Afrika peke yake na Dunia kwa ujumla.
Posted by MROKI On Sunday, February 16, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo