Mpiga
Kura Bi. Habiba Kingazi mkazi wa Mtaa wa Lumumba, Kata ya Ngamiani Kaskazini
akionesha kadi yake baada ya kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura na kupatiwa
kadi mpya katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji TADECO ,Halmashauri ya Jiji la
Tanga.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akishuhudia mwananchi akiboresha taarifa zake.
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele
akimkabidhi kadi ya mpya ya Mpiga Kura Bi. Habiba Kingazi mkazi wa Mtaa wa
Lumumba, Kata ya Ngamiani Kaskazini aliyeboresha taarifa zake katika Daftari la
Kudumu la Mpiga Kura na kupatiwa kadi mpya katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji
TADECO ,Halmashauri ya Jiji la Tanga.
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mikoa ya
Tanga na Pwani limeanza leo leo Februari 13 hadi 19, 2025 na litadumu kwa siku
saba.
********************
Na. Waandishi Wetu, TangaWananchi wa mikoa ya Tanga na Pwani leo Februari 13, 2025 wameanza uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo wananchi wengi wamejitokeza kushiriki katika zoezi hilo.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akishuhudia mwananchi akiboresha taarifa zake.
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele
akishuhudia mwananchi wa Mtaa wa Lumumba, Kata ya Ngamiani Kaskazini aliyekuja
kujiandikisha akichukuliwa picha wakati alipotembelea kituo cha Ofisi ya
Mtendaji TADECO katika Halmashauri ya Jiji la Tanga kushuhudia mwenendo wa
zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambalo limeanza leo
uboreshaji katika mikoa ya Tanga na Pwani. Zoezi hilo litadumu kwa siku saba
kuanzaia leo Februari 13 hadi 19, 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akitazama kitambulisho kikitoka katika Printa.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na mawakala wa vyama.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akishuhudia wananchi wakiwa katika foleni kusubiri kuboresha taarifa zao. Mkazi wa Tanga katika Kata ya Mabawa akisoma bango la maelezo.
Wananchi wakiendelea kuajindikisha na kuboresha Taarifa zao Jijini Tanga.Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omari leo tarehe 13 Februari 2025 ametembelea baadhi ya vituo vya kuandikishia wapiga kura vilivyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani na kushuhudia wananchi wakiendelea kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri leo tarehe 13 Februari 2025 ametembelea baadhi ya vituo vya kuandikishia wapiga kura vilivyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani na kushuhudia wananchi wakiendelea kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira, ametembelea vituo vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, vilivyopo katka Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga leo tarehe 13 Februari, 2025.
0 comments:
Post a Comment