Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akihutubia wakati wa Dua na Maombi ya kuliombea Taifa
kuelekea Miaka 60 ya Muungano yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mkoani
Dodoma tarehe 22 Aprili 2024.Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akihutubia wakati wa Dua na Maombi ya kuliombea Taifa
kuelekea Miaka 60 ya Muungano yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mkoani
Dodoma tarehe 22 Aprili 2024.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akiwa na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa
Dua na Maombi ya kuliombea Taifa kuelekea Miaka 60 ya Muungano yaliyofanyika
katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma tarehe 22 Aprili 2024.
Viongozi
pamoja na Wananchi mbalimbali wakishiriki Dua na Maombi ya kuliombea Taifa
kuelekea Miaka 60 ya Muungano yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mkoani
Dodoma tarehe 22 Aprili 2024.Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akisalimiana na viongozi mbalimbali wa dini mara
baada ya kuhitimishwa kwa Dua na Maombi ya kuliombea Taifa kuelekea Miaka 60 ya
Muungano yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma tarehe 22 Aprili
2024.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akisalimiana na viongozi mbalimbali wa dini mara
baada ya kuhitimishwa kwa Dua na Maombi ya kuliombea Taifa kuelekea Miaka 60 ya
Muungano yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma tarehe 22 Aprili
2024.
*************
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameungana na viongozi wa dini pamoja na watanzania
kwa ujumla katika Dua na Maombi kwaajili ya kuliombea Taifa kuelekea Miaka 60
ya Muungano, Dua na Maombi hayo yamefanyika katika Uwanja wa Jamhuri mkoani
Dodoma leo tarehe 22 Aprili 2024.
Akihutubia mara baada ya maombi na dua ya kuliombea
Taifa, Makamu wa Rais amesema Katika
kipindi cha miaka 60 ya uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Taifa
limeendelea kupiga hatua katika sekta mbalimbali na hivyo kuendelea kuboresha
maisha ya Watanzania.
Amesema tangu Muungano ulipoasisiwa mwaka
1964 umeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka ambapo changamoto mbalimbali za
Muungano zimekuwa zikitatuliwa kupitia mazungumzo ya pamoja na hivyo kujenga
maelewano na mshikamano katika Taifa. Amesema mafanikio hayo ni kutokana na
udugu na ushirikiano wa wananchi wa pande zote mbili za Muungano uliokuwepo
tangu zamani na nia ya dhati ya kujenga
nchi na jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani. Amewasihi wananchi kuendelea kuenzi
na kudumisha tunu za Taifa ambazo ni amani, umoja, mshikamano, utu, haki,
heshima ya mwanadamu, uhuru na demokrasia.
Aidha Makamu wa Rais amesema wakati ikitimia miaka 60 ya
Muungano, bado ni muhimu kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza kasi ya
maendeleo, kukuza ustawi wa jamii na
kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili Taifa. Halikadhalika amewasihi
watanzania wote kwa pamoja kwa kuongozwa na viongozi wa dini, Serikali, wazazi,
walezi na walimu kuwajibika kuendelea kukabiliana na mmomonyoko wa maadili
katika Taifa unaopelekea kuongezeka kwa matendo yanayokiuka mila na desturi za
Kitanzania ikiwemo uhalifu, ukatili, matumizi ya dawa za kulevya na mengineyo
ambayo hayampendezi Mwenyezi Mungu.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amesema serikali
itaendelea kuchukua hatua katika kudhibiti uhalifu na ufujaji wa fedha za umma.
Amewataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo husika pale uovu unapofanyika
katika jamii ili hatua ziweze kuchukuliwa. Ametoa wito kwa Mihimili yote
kufanya kazi kwa ushirikiano kwa manufaa ya nchi na watu wake. Amewasihi
Watanzania kutumikia nchi kwa haki uadilifu na uzalendo.
Vilevile Makamu wa Rais amesema Serikali inatambua na
kuthamini ushirikiano mzuri uliopo baina yake na Taasisi za dini nchini na
itaendeleza ushirikiano huo kwa manufaa na ustawi wa Taifa. Amewashukuru
viongozi wote wa dini nchini kwa kuendelea kuliombea Taifa pamoja na kuendelea
kukemea maovu, kuonya, kufundisha maadili mema na kutoa huduma za kiroho na
kijamii kwa Watanzania. Aidha, amewapongeza
Viongozi wa Dini kwa mchango mkubwa katika kuhakikisha Watanzania
wanaendelea kubaki wamoja na kuendelea kushirikiana licha ya tofauti za dini,
kabila, rangi, ufuasi vyama vya siasa au mahali wanapotoka.
Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema vijana wa sasa wana kisa
sababu kuhakikisha wanaulinda, kuusimamia, kuimarisha na kutetea muungano ili
uendelee kudumu daima na vizazi vijavyo viukute Muungano ukiwa salama na wenye
mafanikio makubwa.
Amesema Muungano unadumisha umoja, amani, mshikamano
na upendo na kutoa uhuru kwa wananchi wa pande zote mbili kuweza kufanya
shughuli za kijamii na kiuchumi.
Dua na Maombi hayo yameongozwa na viongozi wa dini
pamoja na kujumuisha waumini, waimbaji wa muziki wa dini wa kikristo na
kiislamu. Aidha maombi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali
akiwemo Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma, Waziri Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Hamza Hassan
Juma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista
Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, Wabunge pamoja wananchi
mbalimbali.

















0 comments:
Post a Comment