WAZIRI wa Maji Mhe. Juma Aweso (Mb) ametembelea eneo la mradi wa Ujenzi wa nyumba 5000 unaotekelezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika Kijiji cha Msoera Mkoani Tanga hususani kujionea changamoto za upatikanaji wa maji zilizopo katika Kijiji cha hicho.
Aidha, Waziri Aweso amelipongeza Jeshi la Kujenga Taifa kwa kuwa wazalendo katika kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa nyumba kwa ajili ya wananchi wanaohama kwa hiari kutoka Ngorongoro na kuhamia katika kijiji cha Msomera.
Waziri Aweso amesema ameridhishwa na jinsi ya utekelezwaji wa mpango wa kuhakikisha maji yana patikana na kuagiza Mamlaka ya maji ya mkoa wa Tanga kushirikiana na wataalamu kutoka Wizarani kuongeza ujuzi wao ili huduma ya maji iwe bora kwa wananchi wa Msomera.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni bwana Albat Msendo amesema ujio wa Mhe.Waziri Awesu katika kijiji hicho ni chachu kwa wakandarasi kuongeza kasi katika kukamilisha miradi yote ya maji katika eneo hilo.
Akizungumzia namna ya ujenzi wa nyumba unavyoendelea katika Mradi wa Nyumba 5000 Kamanda wa Opareshi hiyo Kanali Sadick Mihayo amesema baada ya kukamisha ujenzi wa hatua ya kwanza nyumba 1000 nguvu yote imeelekezwa kwenye eneo la kitalu F ambako nyumba nyingine 1500 zinaendelea kujengwa.
Jumla ya nyumba Zaidi ya 500 zimekwisha kugaiwa kwa wananchi kutoka Ngorongoro huku wakiendelea kusubiriwa wengine kuja kuhamia.
0 comments:
Post a Comment