Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT Mary Chatanda kuhusu jitihada za kuwawezesha wanawake kutumia nishati safi ya kupikia wakati akikagua mabanda ya maonesho katika Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya Kupikia linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Tarehe 09 Machi 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikagua Jiko linalotumia mkaa mbadala wakati akikagua mabanda ya maonesho katika Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya Kupikia linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Tarehe 09 Machi 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikagua jiko zinazotumia nishati ya gesi na umeme wakati akikagua mabanda ya maonesho katika Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya Kupikia linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Tarehe 09 Machi 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa maelekezo kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha mashine inayosaidia kutengeneza mkaa mbadala inamilikiwa na taasisi mbalimbali nchini wakati akikagua mabanda ya maonesho katika Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya Kupikia linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Tarehe 09 Machi 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya Kupikia linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Tarehe 09 Machi 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifuatilia igizo maalum linalohusu unyanyasaji wa kijinsia na ukataji miti kwaajili ya kupikia wakati wa Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya Kupikia linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Tarehe 09 Machi 2024
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya Kupikia linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk.Doto Biteko, akizungumza katika Kongamano la Wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya Nishati safi ya kupikia lililofanyika leo Machi 9,2024 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, akizungumza katika Kongamano la Wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya Nishati safi ya kupikia lililofanyika leo Machi 9,2024 jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhi vifaa vya nishati safi ya kupikia kwa wawakilishi wa wanawake kutoka kanda mbalimbali nchini wakati wa Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya Kupikia linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Tarehe 09 Machi 2024.
Na.Alex Sonna-DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema katika jukumu alilonalo la kuibeba Ajenda ya Nishati safi ya kupikia barani Afrika itawezesha kuhifadhi misitu na kulinda mazingira nchini.
Mhe. Rais amesema hayo wakati akizungumza kwa njia ya simu na washiriki wa Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya Kupikia linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma.
Amewahimiza wanawake nchini Tanzania kutekeleza yatakayozungumzwa katika kongamano hilo na kuwaahidi serikali itaunga mkono yale yatakayotekelezwa katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Kongamano hilo limewakutanisha wanawake zaidi ya 4000 kutoka Wilaya na Mikoa mbalimbali ambapo pamoja na mambo mengine wanawake hao wamepata fursa ya kujifunza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha nishati safi inapatikana kwa kila Mtanzania.
“Nimeibeba ajenda ya Nishati Safi ya kupikia hapa nchini, nitatafuta fedha kwa ajili ya kukuza matumizi ya nishati safi yakupikia kwa ajili ya wanawake, agenda hii nitaibeba kwa kushirikiana na ofisi ya Makamu wa Rais na Wizzara ya nishati, ” Amesema Mhe.Samia
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema wakati Serikali inakamilisha taratibu za kuanzisha mfuko wa nishati safi ya kupikia ili kuweka ruzuku itakayowawezesha wananchi wa kipato cha chini kumudu bei ya gesi,
''Ni vema wadau mbalimbali kusaidia utekelezaji kupitia mikopo midogomidogo, vikoba au vikundi vya wanawake ili kuhakikisha wanwake wanapata vifaa vya nishati safi."amesema Dkt.Mpango
Aidha ameitaka Wizara ya Fedha kutazama uwezekano wa kupitia viwango vya kodi kwa majiko yanayotumia nishati safi ya kupikia ili wananchi waweze kumudu kununua majiko hayo kwa urahisi.
Makamu wa Rais amehimiza vijiji na watu binafsi wanaopata mapato kutokana na biashara ya kaboni kutumia mapato hayo kugharamia nishati safi ya kupikia.
Hata hivyo ametoa wito kwa taasisi za utafiti, sekta binafsi na wadau wengine kubuni teknolojia rahisi na zitakazopatikana kwa gharama nafuu ili kuharakisha uhamaji kutoka kwenye matumizi ya nishati chafu.
Amesema teknolojia zinazohitajika ni pamoja na zile za kupata majiko yanayotumia nishati safi kuwezesha kupika chakula kinachoiva kwa muda mrefu kama maharage na kande badala ya kutumia mkaa au kuni.
"Nitoe wito kwa sekta binafsi kuunga mkono na kuchangia katika kampeni ya kuondokana na matumizi ya nishati chafu. Amesema ni muhimu Sekta binafsi kutumia mifuko ya Wajibu kwa Jamii kuwezesha kaya na taasisi zinazowazunguka kupata nishati safi ya kupikia mjini na vijijini."amesema Dkt.Mpango
Pia amewataka wito wadau wote kuandaa programu mbalimbali zitakazotoa elimu na hamasa kwa jamii nchi nzima ili kuongeza uelewa juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Ameviasa vyombo vya habari na Asasi za kiraia kuibeba ajenda ya nishati safi ya kupikia na kuwa mstari wa mbele katika kuielezea kwa umma wa Watanzania.
"Vyombo vya habari vinao wajibu muhimu wa kuelezea umma kuhusu madhara ya kuendelea kutumia nishati chafu ikiwemo kupoteza misitu, mmomonyoko wa udongo, kuongeza gesijoto, magonjwa ya mfumo wa hewa na madhara ya kiuchumi kama watoto wa kike kushindwa kumaliza masomo. "amesema
Makamu wa Rais amesema Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa kipaumbele cha juu kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia hapa nchini kwenye ajenda ya Taifa ya maendeleo pamoja na kuongeza rasilimali kuhakikisha ajenda hiyo inafanikiwa.
Amesema Rais amefanya maamuzi makubwa ikiwemo kuunda Kamati ya Kitaifa itakayosimamia utekelezaji wa ajenda hiyo, kuanzisha mfuko wa nishati safi ya kupikia ili kuweka ruzuku itakayowawezesha wananchi wa kipato cha chini kumudu bei ya gesi na kuchagiza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa taasisi za Serikali zinazohudumia watu zaidi ya 100 kwa siku.
Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk.Doto Biteko amezitaka kampuni zinazojihusisha na uzalishaji wa mitungi ya gesi ya kupikia kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia nchini.
Amesema kampeni ya nishati safi ya kupikia ni ya nchi nzima na safari yake ilianzishwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan baada ya kuzindua mpango wa nishati safi ya kupikia kwa wanawake wa Afrika akiwa katika mkutano wa kidunia.
Aidha amewaomba viongozi wa Serikali pamoja na taasisi kuelewa kwamba ajenda ya nishati safi sio ya Serikali peke yake bali ni ajenda ya wote, hivyo waisukume kuhakikisha mwanamke wa Tanzania anapata hadhi
Dk. Biteko pia ametumia nafasi hiyo kuwaomba wanaume wote nchini kujipa wajibu wa kutimiza majukumu yao kwenye familia ikiwemo kuwezesha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kuwezesha wanawake kupika kwa urahisi na kuokoa afya zao kutokana na moshi wa kuni.
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema kuwa kuanzia Julai mwaka 2021Wizara hiyo imekuwa mstari wa mbele kutekeleza maelekezo ya Serikali yaliyotolewa na Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuwa ifikapo mwaka 2023 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.
Amesema pia hatua ya Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa nishati safi ya kupikia kugawa majiko ya gesi pamoja na majiko banifu ni muendelezo wa juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha ifikapo mwaka 2033 zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania(UWT)Mary Chatanda,amemshukuru Rais Samia kwa maono yake juu ya kongamano hilo na kueleza kuwa litawezesha kuwatua wanawake kichwan kuni na kuwapa nafasi ya kutumia muda wao mwingi kwenye shughuli za kijamii.
Amesema kupitia mfuko wa Nishati umesaidia kuboresha huduma za nishati kwa gharama zenye ubora kwa watu wa chini na kuiomba Serikali kuona namna ya kuwezesha gesi ya majumbai kupatikana kwa gharama nafuu na kuwezesha majiko yanayotolewa kutumika kama ilivyokusudiwa.
‘Tumeona Serikali ikipambana na utunzaji mazingira na kutenga Baheti ya nishati safi ya kupikia kwa mwaka wa fedha 2024,hatua hii itasukuma wanawake kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa na kulinda mazingira na afya na kuwa na muda wa kutosha kufanya shughuli za uzalishaji mali,”amesisitiza na kuongeza;
Sisi wanawake tunakwenda kuwa wadau wa mazingira kupitia nishati safi ya kupikia na kuwezesha wanawake wengine kuacha kutumia kuni ili kulinda uhifadhi wa mazingira”amesema.
0 comments:
Post a Comment