Nafasi Ya Matangazo

April 24, 2023

Na Patricia Kimelemeta
WATOTO wawili Abrahaman Kareem  Chamwande (6)  na Kauthar Kareem Chamwande, (3) wamefariki Dunia baada ya kudaiwa kunyeshwa sumu na baba yao mzazi Kareem Chamwande.

Tukio hilo limetokea maeneo ya Chanika Manispaa ya Ilala Jijini Dar Es Salaam hali iliyosababisha huzuni kwa ndugu na jamaa walikua karibu na familia hiyo.

Hata hivyo, Serikali  inatekeleza Programu Jumuishi ya Kitaifa  ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) ambayo imeanza 2021 na kumalizika 2026.inalenga  kusimama malezi yao katika afua tano za ulinzi na usalama, afya, elimu, lishe na michezo.

Programu hiyo inalenga watoto kuanzia umri sifuri hadi miaka minane ambayo inashirikisha Serikali na Asasi za kiraia Katika utekelezaji wake.

Hata hivyo, katika hali ya kusikitisha, watoto hao wanadaiwa  kufanyiwa ukatili huo na baba yao mzazi kwa kuwanyesha juisi inayosadikiwa kuwa na sumu.

Mazishi ya watoto hao wawili yamefanyika katika makaburi ya kwa mwarabu Chanika Mwisho, ambapo inadaiwa kuwa baba wa watoto hao anashikiliwa na Jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi mara baada ya kutokea kwa tukio hilo ambapo  alijaribu  kujiua kwa kutumbukia kwenye shimo la choo lakini ilishindikana.

Hata hivyo,  Polisi waliwahi kufika kwenye eneo la tukio hilo  kwa kushirikiana na raia wema na kufanikiwa kumuokoa.

Inadaiwa kuwa,  wazazi wa watoto hao Zubeda Ngwale na Chamwande walikuwa wametengana takribani mwaka mmoja uliopita na watoto hao wawili walikua wakiishi na baba yao.

Baadhi ya majirani walioshuhudia tukio hilo wamedai kuwa, watoto hao walifanyiwa ukatili huo usiku wa kuamkia jumapili ambapo baba yao aliwapa juisi inayodaiwa kuwa na sumu.

" Wazazi wa watoto hawa walikuwa wametengana, baba yao alienda kuwachukua na kuwalea, lakini mama yao aligoma kurudi kwa mumewe na kumwambia hamtaki tayari ameshapata mwanaume mwingine, hivyo aliwataka watoto wake awachukue na kwenda kuwalea kwa mume mwingine," alisema shuhuda.

Shuhuda mwingine alidai kuwa, Zubeda na Kareem walibahatika kupata watoto watatu, aliamua kuondoka kwa mumewe na kurudi nyumbani kwao kwa madai kuwa  mumewe alikua akimpiga mara Kwa mara. 

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kwa kushirikiana na mamlaka nyingine na kwa sasa wapo katika  hatua ya kukamilisha na kujua chanzo cha mauaji hayo.

"Tunamshikilia Kareem ( baba wa marehemu) ambaye anadaiwa kuwaua watoto wake wawili kwa kuwapa juisi yenye sumu na sasa tunashirikiana na Mamlaka zetu za kisayansi kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo Ili tukimaliza aweze  kufikishwa Mahakamani wakati wowote kuanzia sasa”

Programu ya PJT- -MMMAM inalenda kusimama Malezi ya watoto kuanzia umri sifuri hadi miaka minane Ili kuhakikisha kuwa, watoto wanalelewa katika hali ya utimilifu  na kupata lishe bora, afya, elimu, Malezi yenye mwitikio na ulinzi na usalama.

Takwimu zinaonyesha kuongezeka kwa kesi za ukatili wa watoto Katika umri wa kuanzia miaka mwili na kuendelea ambapo watoto wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa kingono, kimwili na kutelekezwa.

.Juni 2022,Waziri wa Maendeleo ya Jamii, WanawakeJinsia na Makundi Maalum Dk. Doroth Gwajima akitoa  takwimu ya matukio ya ukatili kwa watoto katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2021,  amesema, jumla ya matukio yaliyoripotiwa ndani ya Jeshi la Polisi ni 11,499 ikilinganishwa na matukio 15,870 katika kipindi kama hicho mwaka 2020, sawa na upungufu wa matukio 4,371 ikiwa na asilimia 27.5

Amesema kuwa Mikoa iliyoongoza  ni Arusha (808), Tanga (691), Shinyanga (505), Mwanza (500) na Mkoa wa Kipolisi Ilala (489). Akisema makosa yaliyoongoza kwa idadi kubwa ni ubakaji (5,899), mimba kwa wanafunzi (1,677) na ulawiti (1,114)
Posted by MROKI On Monday, April 24, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo