Bi. Tuma Daniel Abdallah kuwa Mhariri Mkuu wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ********
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia
Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:
i) Amemteua Mhandisi
Bashir Juma Mrindoko kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Shirika la Utafiti wa
Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO). Mhandisi Mrindoko ni Katibu Mkuu Mstaafu.
ii) Amemteua Prof. Shabani
Athumani Chamshama kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu
Tanzania (TaFF). Prof. Chamshama ni Profesa wa Sayansi ya Misitu na Mhadhiri
Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Morogoro.
iii) Amemteua Bi. Sarah Kinyamfura
Barahomoka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Promotion of Rural
Initiatives and Development Enterprises Limited (PRIDE). Bi Barahomoka ni
Mwandishi Mkuu wa Sheria Mstaafu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
iv) Amemteua Bw. Paul
Thomas Sangawe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Self
Microfinance (Self -MF). Bw. Sangawe ni Mkurugenzi wa Sera na Utaratibu wa
Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dodoma.
v) Amemteua Dkt. Oswald
Jotam Masebo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Makumbusho ya Taifa
(NMT). Dkt. Masebo ni Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
vi) Amemteua Prof.
Emmanuel Amaniel Mjema kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM). Prof. Mjema ni Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara
(CBE), Dar es Salaam.
vii) Amemteua
Bi. Tuma Daniel Abdallah kuwa Mhariri Mkuu wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali
(TSN). Bi. Abdallah alikuwa Kaimu Mhariri Mkuu wa Kampuni ya Magazeti ya
Serikali (TSN).
Uteuzi huu
unaanza mara moja.
Posted by MROKI
On Wednesday, June 29, 2022
No comments
0 comments:
Post a Comment