Nafasi Ya Matangazo

April 02, 2026

DODOMA
Kuelekea sikukuu ya Pasaka, Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Bw. Pendolake Elinisafi, ameongoza ziara ya kutembelea kaya za watu wenye ulemavu wa macho wilayani Chamwino (Matembebora), akiongozana na Meneja Msaidizi Huduma kwa Walipa Kodi, Bw. John Njau, pamoja na watumishi wengine wa TRA Mkoa wa Dodoma, kwa lengo la kutoa faraja, upendo na kuwajengea matumaini, akisisitiza kuwa wao ni sehemu muhimu ya jamii inayothaminiwa.

Akizungumza kwa niaba ya wanakaya hao, Mwenyekiti Bw. Yeledi Cheleso ameishukuru TRA Dodoma kwa moyo wa kujali na msaada walioutoa, akieleza kuwa hatua hiyo imeongeza faraja na kuwapa nguvu mpya ya kuendelea na maisha.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii, Bi. Elizabeth, ameipongeza TRA kwa kuendeleza mshikamano na jamii, akibainisha kuwa juhudi hizo zinaimarisha ushirikiano kati ya taasisi na wananchi, hususan kwa makundi yenye uhitaji maalum.

Ziara hiyo imeacha ujumbe wa upendo na mshikamano, ikionesha dhamira ya TRA ya kuendelea kugusa maisha ya jamii sambamba na majukumu yake ya ukusanyaji wa mapato.
Posted by MROKI On Thursday, April 02, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo