Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ametaja hatua zitakazochukulia na
Tanzania katika kuboresha haki za kiuchumi kwa wanawake.
Makamu wa Rais ameyasema hayo katika Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa (Generation
Equality Forum) linalofanyika Paris Ufaransa.
Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
Makamu wa Rais amesema Tanzania inachukua hatua muhimu ili kukuza na kulinda
haki za kiuchumi kwa wanawake.
Mheshimiwa Makamu wa Rais amezitaja hatua hizo ni pamoja na kuongeza vituo vya
kulea watoto mchana katika maeneo mbalimbali ya shughuli za kiuchumi kama vile
sokoni na maeneo mengine ya kazi .
Makamu wa Rais amesema serikali inachukua hatua za kuongeza upatikanaji wa
huduma muhimu za kijamii kama vile umeme, maji pamoja na nishati mbadala ili
kuwapunguzia wanawake mzigo wa majukumu mengi katika maeneo ya vijijini na
baadhi ya mjini.
Aidha amesema serikali itaongeza upatikanaji wa teknolojia rahisi na sahihi ili
kuongeza tija na ufanisi katika shughuli zinzazofanywa na wanawake katika
uzalishali mali.
Makamu wa Rais amesema hatua nyingine ni pamoja na kuongeza fursa za elimu kwa
wanawake ikiwemo kuanzisha shule za sayansi kwa wasichana, elimu ya ufundi
stadi ili kuwapatia ujuzi na stadi zinazowezesha kuzalisha kwa tija.
Hatua nyingine ni pamoja na kuwawezesha wanawake kumudu na kutumia teknolojia
za kidijitali kwaajili ya kuongeza ushindani katika uzalishaji na shughuli zao
mbalimbali za kiuchumi.
Kuwawezesha wanawake kupata afua za kifedha kwa kutumia ubunifu wa aina
mbalimbali ikiwemo kutumia njia za kielektroniki.Kuondoa fikra na tamaduni
potofu zinazozuia wanawake kujihusisha na shughuli za kiuchumi ikiwemo umiliki
wa ardhi.
Kupanua wigo wa huduma za hifadhi ya jamii ili kujumuisha kaya ambazo zipo nje
ya uchumi rasmi.
Urasimishaji wa biashara zenye staha zinazofanywa na wanawake ili kuweza kupata
huduma za kifedha.Kuimaraisha mifuko ya uwezeshaji wanawake kiuchumi ili
kurahisisha kupata mitaji ya kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Mara baada ya kuwasilisha ahadi hizo, Makamu wa Rais amekutana na kufanya
mazungumzo na Dkt. Phumzile Mlambo Ngcuka Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake (Un- Women).
Dkt Phumzile amesema amefurahishwa na ahadi zilizotolewa na serikali ya
Tanzania katika kuchagiza haki za kiuchumi za wanawake na kumpongeza makamu wa
Rais kwa uwakilishi mzuri. Makamu wa Rais amemuhakikishia Dkt Phumzile kwamba
Tanzania itaendelea kusimamia na kulinda haki za kiuchumi za wanawake.
0 comments:
Post a Comment