Naibu
Spika Dr. Tulia Ackson (katikati) akizungumza na wahitimu wa Akademi ya
Filamu ya MultiChoice (MultiChoice Talent Factory Academy) nje ya
ukumbi wa bunge jijini Dodoma jana.
Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka
bara la Afrika walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu
yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika. Kutoka kushoto ni Jane Moshi,
Sarah Kimario, Jamal Mohamed na Wilson Nkya
Wanafunzi
wanne waliohitimu hivi karibuni mafunzo maalum ya uzalishaji filamu
chini ya programu ya MultiChoice Talent Factory wamehudhuria kikao cha
bunge la Tanzania kama wageni
maalum wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.
Katika
ziara hiyo pia wanafunzi hao walikutana na wadau mbalimbali akiwemo
naibu spika Dr. Tulia Akson waziri Dr. Harrison Mwakyembe, naibu waziri
Juliana Shonza, naibu waziri Anthony
Mavunde na katibu mkuu wa wizara Suzan Mlawi.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe
akisalimiana na wahitimu wa Akademi ya Filamu ya MultiChoice
(MultiChoice Talent Factory Academy) katika viwanja
vya bunge jijini Dodoma jana. Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni
miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika walioshiriki mafunzo
maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika.
Kutoka kulia ni Sarah Kimario, Jamal Mohamed, Wilson
Nkya, Jane Moshi pampja na mkuu wa Mahusiano wa MultiChoice Tanzania
Johnson Mshana
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti na wahitimu hao katika viwanja vya bunge jijini
Dodoma, viongozi hao waliwataka wahitimu hao kutumia mafunzo maalum
waliyoyapata katika kuleta mapinduzi
ya tasnia ya filamu hapa Tanzania.
Naibu
waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza (kushoto)
akizungumza na wahitimu wa Akademi ya Filamu ya MultiChoice (MultiChoice
Talent Factory Academy) katika
viwanja vya bunge jijini Dodoma jana. Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania
ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika walioshiriki mafunzo
maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika.
Kutoka kulia ni Wilson Nkya, Grace Mgaya, Jane
Moshi, Sarah Kimario na Jamal Mohamed.
Kwa
pamoja wamekiri kuwa tasnia ya filamu ni moja ya tasnia zinazokuwa kwa
haraka hapa nchini hivyo ni muhimu wanatasnia wawe na mafunzo ya kutosha
na yanayoendana na wakati ili
iweze kupambana na nchi nyingine katika soko la filamu ulimwenguni huku
tukihakikisha kuwa kazi zetu zinaakisi mila, desturi, utamaduni na
uzalendo wetu.
Akizungumza
na wanafunzi hao baada ya kumtembelea ofisini kwake, Katibu Mkuu Suzan
Mlawi amesisitiza ahadi ya serikali kushirikiana na wadau wa tasnia
mbalimbali ili kuharakisha
ukuaji wa tasnia hizo. Amesema ushirikiano kati ya serikali na wadau ni
muhimu na kwamba serikali itaendelea kuhakikisha kuwa sera na kanuni
zinaboreshwa ili kuakisi hali halisi ya ukuaji wa tasnia ya filamu.
Wanafunzi
hao wanne – Wilson Nkya, Jane Moshi, Jamal Mohamed na Sarah Kimario
wamehitimu mafunzo maalum ya mwaka mmoja yanayofadhiliwa na MultiChoice
ambapo vijana 60 kutoka kote
barani Afrika huchaguliwa kwa mafunzo hayo kutoka nchi mbalimbali.
Programu hiyo ina vituo vitatu vya mafunzo ambapo kwa upande wa kusini
mwa Afrika kipo Lusaka Zambia, kwa Afrika Mashariki na kati kipo Nairobi
Kenya na kwa Afrika Magharibi Lagos Nigeria.
Mkuu
wa Mahusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (wa pili kushoto)
akiwatambulisha wahitimu wa mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu kwa
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe (Kushoto) mara baada ya wahitimu hao
kuhudhuria kikao cha bunge kama wageni maalum wa waziri. Wanafunzi hao 4
kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika
walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa
filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika kupitia program yake ya
MultiChoice Talent Factory. Kutoka kulia ni Sarah Kimario, Jamal
Mohamed, Wilson Nkya, Jane Moshi pampja na Afisa Uhusiano wa MultiChoice
Tanzania Grace Mgaya
Awamu
ya pili ya program hii itaanza mwezi Octoba 2019 ambapo wanafunzi
wengine 60 watapata mafunzo hayo. Tanzania kwa mara nyingine tena
itapeleka wanafunzi wanne.
0 comments:
Post a Comment