Nafasi Ya Matangazo

September 20, 2019


Mwandishi wetu,Arusha
Timu ya soka ya Kakoi ya wilaya ya Babati mkoa wa Manyara,imefanikiwa kuingia  robo fainali katika michuano ya Chemchem CUP ambayo inafanyika wilayani Babati baada ya jana timu ya Kazamoyo kushindwa kutokea uwanjani .

Katika michuano hiyo, ambayo inaendelea katika eneo la Mdori, jumla ya timu 20 za soka zinashiriki na timu nne za mpira wa pete ambapo kiasi cha  sh 70 milioni zimetolewa na  Taasisi ya uhifadhi ya Chemchem kuendesha michuano hiyo.

Timu ya Kakoi amefanikiwa kutinga robo fainali baada ya kujipatia pointi tatu jana na kufanya kuongoza kundi lake, ambapo awali iliitandika timu ya Kona Mbaya magori 5-0.

Wafungaji katika mchezo huo, walikuwa ni Devis Severine ambaye alifunga magori matatu , Shaban Jabu gori moja na Buzuka Amani gori moja.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Katibu wa michuano hiyo, Beno Alfred alisema  michuano hiyo,  inashirikisha jumla ya timu kutoka vijiji 10, ambavyo vinaunda  jumuiya ya  jamii ya uhifadhi ya wanyamapori ya  Burunge. 

"katika  michuano hiyo, kuna makundi manne ambapo timu mbili kutoka kila kundi zinasonga mbele kwa ajili ya kuingia robo fainali.

Mratibu wa michuano hiyo wa Taasisi ya Chemchem ambayo imewekeza shughuli za kitalii katika hifadhi hiyo, Walter Pallanyo, alisema kiasi cha milioni 4.5 kinatarajiwa kutolewa kama zawadi kwa washindi.

Pallangyo alisema timu zote ambazo zinashiriki, zilipewa jezi na mipira kwa ajili ya michuano hiyo ambayo hufanyika kila mwaka.

"lengo la michuano hiyo ni kuwashirikisha vijana  katika  vita dhidi ya ujangili   lakini pia kujua thamani ya uhifadhi wa maeneo yao kwa shughuli za kitalii"alisema 

Timu ya Manyara ndio ilitwaa ubingwa katika michuano ya Chemchem mwaka jana.

Timu za mpira wa pete ambazo zinashiriki ni  timu ya Mwada, Mdori, Walimu na Ngolei 
Posted by MROKI On Friday, September 20, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo