Mbunge wa jimbo la Same Magharibi, Dk. Mathayo David
Mathayo akikabidhi Mabati 200 kwa uongozi wa kata ya Vudee kama alivyoahidi kwa
ajili ya ujenzi wa madarasa na zahanati ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya
uchaguzi yam waka 2015-2020 mbele ya wananchi wa kata hiyo
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Dk.Mathayo David Mathayo akimkabidhi diwani wa
kata ya Bangalala, George Mshana mipira
kwa ajili ya ligi itakayoshindanisha vijiji vyote ambapo mshindi kwa upande wa
wanawake atapatiwa shilingi milioni mbili na wanaume timu mshindi atapatiwa
shilingi milioni mbili wakati wa mkuatano wa hadhara ikiwa ni muendelezo wa
ziara yake ya utekelezaji wailani ya uchguzi ya CCM mwaka 2015-2020 kama
alivyoahidi kwa jailia ya kata hiyo.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Dk.Mathayo David
Mathayo akimkabidhi fedha taslim diwani wa kata ya Bangalala George Mshana mbele ya wananchi wa kata hiyo wakati
wa mkuatano wa hadhara ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya utekelezaji wailani
ya uchguzi ya CCM mwaka 2015-2020 kama alivyoahidi kwa jailia ya kata hiyo.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi, Dk Mathayo David
Mathayo akikabidhi mifuko ya saruji kwa uongozi wa kata ya Vudee kama
alivyoahidi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na zahanati ikiwa ni utekelezaji wa
ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020 mbele ya wananchi wa kata hiyo
Mbunge wa jimbo la Same
Magharibi Dk. Mathayo David Mathayo akiwakabidhi fedha za ujenzi wa
madarasa,ununuzi wa viti na mahitaji mengine walimu wakuu wa shule za msingi na
sekondari wa kata ya vudee Bukuri Masago na diwani wa kata hiyo Vudee Ngomoi
Ntarishwa ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020 kama
alivyoahidi kwa jaili ya kusaidia maendeleo ya elimu katika kata hiyo.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Mathayo David
Akihutubia wananchi wa kata ya Vudee katika jimbo la Same Magharibi wakati wa
ziara yake katika kata hiyo ikiwa ni mfululizo wa utekelezaji wa ilani ya
uchaguzi alizoahidi.
***************
MBUNGE wa jimbo la Same
Magharibi Dk.Mathayo David Mathayo ameendelea na ziara yake ya kutekeleza ilani
ya uchaguzi katika jimbo lake huku akija na staili mpya ya kutatua kero za
wananchi kwa mtindo wa papo kwa papo.
Licha ya kutekeleza ahadi
alizoahidi wakati akiomba ridhaa ya kuwaongoza wananchi wa Same Magharibi
mbunge huyo amekuwa akitekeleza wakati mwingine kutoa fedha taslim pale anapoombwa na wananchi wa kata husika
nje ya ahadi anazotekeleza katika kila kata.
Akizungumza na wananchi
wa kata ya Vudee na Bangalala mbele ya mbunge huyo diwani wa Kata hiyo Ngomoi
Ntarishwa pamoja na kumshukuru mbunge huyo kwa utekelezaji wa ahadi zote
alizoahidi wakati akiomba ridhaa ya kuwaongoza wanachi hao.
“mhe mbunge wananchi wa
Vudee wanakushukuru sana kwa utekelezaji wa ahadi uliahidi na umetekeleza,sisi
wanannchi wa Vudee tuna Imani kubwa na wewe hivyo pamoja na kuwa umetelekeza
bado tuna changamoto kadhaa ambazo tunaomba pia utusaidie”alisema Ntarishwa
Mbunge huyo ambae licha
ya kutekeleza ahadi za mabilioni amekuwa akipandwa na mzuka pale wananchi wake
wanapomlilia shida na kuhakikisha hawaachi hivyo hivyo wala kuahidi bali
amekuwa akizitatua papo kwa papo.
“Ndugu zangu leo
nimekuja kutekeleza ahadi zote nilizoahidi wakati nilipokuja kuwashukuru kwa
ushindi wa kishindo ambao mlinichagua,lakini nasikia kuna watu wanapitapita
wakisema kuwa Mathayo hajarudi,hivi niwaulize swali ilani inatekelezwa ndani ya
kipindi gani,si ni kwa miaka mitano?hivi mtoto akiaanza shule akafika kidato
cha pili utasema basi kabla hajafika kidato cha nne?,” alizungumza kwa kuhoji
Mathayo.
Mathayo amewataka
wananchi hao kutokubali kurubuniwa na
kuendelea kuwa na Imani na chama cha mapinduzi ambacho kupitia Rais John
Magufuli kimeleta maendeleo makubwa kwa wananchi wake tangu serikali ya awamu
ya tano iingie madarakani.
Akiwa katika kata ya
Vudee na Bangalala mbunge huyo ametekeleza ahadi zake kwa kutoa mifuko ya fedha
taslimu saruji 350 kwa ajili ya ujenzi
wa shule,zahanati,vyoo vya wanafunzi,,mabomba ya maji,mabati 200,matanki ya
maji,comyuta,mashine za photokopi,mipira ya kuchezea,key bord,nondo,meza na
viti,huku akiahidi kuleta katapila kwa ajili ya ujenzi wa barabara korofi ya
Kisesa,vyote kwa ajili ya kata ya Vudee.
Baadhi ya ahadi mpya
alizozitoa na kuzitatua papo kwa papo katika kata ya Vudee ni kompyuta,mashine
ya photokopi,jiko la shule ya sekondari masheka,mabati 30,na upande wa zahanati
ya kiji cha kisesa bati 100.
Ombi jingine
alilolitekeleza papo kwa papo katika kata ya Bangalala ni kukubali kutoa gari
la kubebea wagonjwa kwa ajili ya kata hiyo, kuleta katapila kwa ajili ya
kutengeneza barabara za kata hiyo,tenki la kuhifadhia maji,ambapo pia ametoa
fedha taslimkwa ajili ya kunua mipira ya maji 20 na nyinginezo.
0 comments:
Post a Comment