Nafasi Ya Matangazo

May 08, 2019

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, akipokea mkataba wa huduma kwa wateja wa Mamlaka ya Mwasiliano Tanzania (TCRA) baada ya kuuzindua jijini Dodoma leo. 
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe (wapili kushoto) akikabidhi mkataba wa huduma kwa wateja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Dk. Jones Killimbe baada ya uzinduzi wa mkataba huo jijini Dodoma leo. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa Mkataba wa Huduma ya Mteja jijini Dodoma leo. 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba alisema Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA umelenga kuboresha utoaji wa huduma, kutatua malalamiko ya watumiaji wa huduma za mawasiliano na utadhibiti vitendo vya rushwa kwenye sekta ya mawasiliano nchini.

“ TCRA ilishirikiana wataalamu wa masuala ya rushwa kutoa elimu kwenye mikoa kwa wadau kwenye mikoa 17 ya Tanzania Bara na Zanzibar na maoni yao yakaingizwa kwenye mkataba. Ukweli na uwazi kupitia mkataba huo ndio utakaowezesha kutatua vitendo vya rushwa na upatikanaji wa taarifa sahihi.

Alisema mkataba huo ni maafikiano ya kijamii ambapo TCRA inaafikiana na wateja wake pamoja na watumishi kuhakikisha huduma zinazotolewa zinazingatia haki na wajibu kwa mteja na kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha maendeleo yanafikiwa kwa kuzingatia maadili na sheria za nchi.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa Mkataba wa Huduma ya Mteja wa TCRA 
Kamwele amesema mkataba wa huduma kwa mteja wa TCRA uliozinduliwa leo, ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, ambayo imekuwa ikisisitiza usalama kwenye njia za mawasiliano.

Amsema kutokana na umuhimu wa mkataba huo, TCRA inatakiwa kusimamia makubalino hayo ili sekta ya mawasiliano iendelee kutoa mchango katika kukuza uchumi.

“Kutokana na umuhimu wa mkataba huu katika kudumuisha mawasiliano,ninaagiza TCRA kuendelea kutoa elimu kwa umma na kusimamia makubaliano haya ili sekta wa mawasiliano iendelee kutoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Watanzania.

“ Niwaombe Wananchi kuendelea kutumia huduma za mawasiliano kwa manufaa ili kuweza kuboresha maisha yetu na kutuletea maendeleo.”
 Sehemu ya wakazi wa jiji la Dodoma kutoka kada mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo wakifuatilia matukio. 

  Sehemu ya wakazi wa jiji la Dodoma kutoka kada mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo wakifuatilia matukio. 

 Manaibu Waziri kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashsta Nditiye (kulia) anaeshughulika na Uchukuzi na Mawasiliano na Elius Kuandika anaeshughulika na Ujenzi wakiwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza wakiwa katika uzinduzi huo. 
 Meza kuu ikiongozwa na Mgeni Rasmi, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiuliano, Isack Kamwele (wanne kulia) 
 Meza kuu ikiongozwa na Mgeni Rasmi, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiuliano, Isack Kamwele (wanne kulia) 
Posted by MROKI On Wednesday, May 08, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo