Nafasi Ya Matangazo

January 14, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu 
Hassan amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe.

Daniel Godfrey Chongolo, kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya
Mbozi Mhe. Bi. Ester Alexander Mahawe. 

Marehemu Mahawe amefariki leo tarehe 14 Januari, 2025 katika hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro ambako alikuwa akipatiwa matibabu. 

Rais Dkt. Samia anawapa pole familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Mahawe.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Mahawe mahala pema peponi, Amina.
Posted by MROKI On Tuesday, January 14, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo