Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Eng. Isack Kamwelwe (hayuko pichani), ameipongeza Bodi na Menejimenti ya TCRA kwa kuwa mfano bora kwa taasisi nyingine za umma kuandaa Mkataba wenye lengo last kuboresha huduma.
Waziri Kamwelwe amempongeza Mkurugenzi mkuu wa TCRA, Eng. James Kilaba (katikati) kwa ubunifu na umakini mkubwa katika kufanikisha uandaaji wa mkataba huo utakaowafanya watanzania wajivunie huduma bora na kujaliwa katika taifa lao.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe (wapili kushoto) akikabidhi mkataba wa huduma kwa wateja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Dk. Jones Killimbe baada ya uzinduzi wa mkataba huo jijini Dodoma leo. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba.
Waziri Kamwelwe amesema kuwa uboreshaji wa huduma za Mawasiliano nchini pia utasaidia kuondoa rushwa kabisa kwani katika e-government, mteja atahudumiwa pasipo kuonana na mtoa huduma uso kwa uso.
"Ni katika kuonana uso kwa uso vitendo vya rushwa vinafanyika, katika simu ukioomba rushwa utamulikwa tu," alisema.Tanzania chini ya Rais Magufuli, inapigiwa mfano katika bara la Afrika kwenye vita dhidi ya rushwa.
Akiongea katika hafla hiyo kubwa iliyofanyika katika ukumbi ya Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe George Mkuchika, amezitaka taasisi nyingine zote za umma kuiga mfano wa TCRA na kuandaa mikataba ya wateja.
Ameitaka Mamlaka hiyo kuutekeleza Mkataba huo ili kusaidia kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini, hasa ukizingatia unyeti wa sekta ya Mawasiliano.
Naye Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, mbali na kuipongeza TCRA kwa kazi nzuri ya kuwahudumia watanzania, ameishukuru Mamlaka kwa mahusiano mazuri ya kikazi baina yao.
Hafla hiyo imehudhuriwa viongozi mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Eng. Atashasta Nditiye na Naibu mwingine katika Wizara hiyo, anayeshughulikia sekta ya Ujenzi, Eng. Elias Kuandikwa.
Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Eng. Mary Sassabo, Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo, Dk Jim Yonazi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
0 comments:
Post a Comment