Nafasi Ya Matangazo

April 23, 2019

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela akigawa misaada kwa wananchi wenye uhitaji katika kanisa la ufufuo na uzima tawi la Iringa
 Baadhi ya waumini wakifuatilia utoaji wa misaada kwa watu wenye uhitaji katika kanisa hilo
Na Fredy Mgunda, Iringa
Zaidi ya kaya 150 zisizo na uwezo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa zinazojumuisha Wajane,watoto Yatima na Wagane zimepewa msaada wa chakula chenye thamani ya shilingi Million 4 msaada uliotolewa na kanisa la Ufufuo na Uzima Tawi la Iringa ili waweze kusheherekea sikukuu ya Pasaka.

Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwaomba wananchi wenye kipato kikubwa kuhakikisha wanajitolea kuwasaidia wananchi ambao hawana uwezo wa kupata mahitaji muhimu.

“Wilaya ya Iringa inakabiriwa na wananchi ambao ni masikini kabisa na kuwa wananchi ambao wote wana kipato kizuri na kikubwa ,hivyo nawaomba wananchi wenye kipato wajitolee kuwasaidia hawa ambao hawapati mahitaji muhimu” alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa dunia kote hakukosekani wananchi wahitaji hivyo hata wilaya hii inawananchi wa namna hiyo na serikali inaendelea kupandana kuhakikisha wananchi hao wanatoka kwenye eneo hilo na kuanza kujitegemea.

“Wilaya ya Iringa kuna mzunguko mkubwa wa kipato hivyo lazima tuwasaidie hawa wahitaji wa mahitaji muhimu kwa lengo la kuundoa umasikini wilayani kwangu” alisema Kasesela

Aidha kasesela alisema kuwa wananchi wanatakiwa kupewa msaada mara tatu tu baada ya hapo anatakiwa kuanza kujitegemea kutoka na ule msaada ambao alikuwa anapewa kwa awamu tatu ambazo zinamsaidia kukijikomboa kimaisha.

“Msaada unatolewa mara tatu tu baada ya hapo inatakiwa mhitaji huyo aanze kujitegemea na kuondoa uzembe uliopo kwenye vichwa vya wananchi hao hasa wilaya ya Iringa lazima wananchi wangu waondokane ha hiyo kasumba” alisema Kasesela

Naye mchungaji wa kanisa la Ufufuo na Uzima Tawi la Iringa Bruno Masawe alisema kuwa mapango wa kanisa ni kuhakikisha inawahudumia wananchi ambao hawa uwezo na kuwapa maarifa ya kukuza kipato na kuacha kuwa tegemezi hapo baadae.

“Mungu alituagiza kuwa siku ya pasaka ni siku ya kutoa hivyo hata sisi kama kanisa la lawachristo tunatakiwa kuwakumba wananchi wa aina hiyo kwa lengo la kuahikisha tunawakumba wananchi hao ambao hata mungu kautajiza hivyo” alisema Kasesela

Kwa upande baadhi ya wananchi waliopata msaada huo walilipongeza na kulishukuru kanisa la Ufufuo na Uzima Tawi la Iringa kwa kuwakumbuka na kuwapa msaada huo ambao utawasaidia kuendesha maisha yao kwa kiasi furahi.

“Hali ya uchumi ni ngumu kwa sasa hivyo kupewa msaada huu wa vyakula na nguo umetusaidia sana na tunaishukuru serikali pamoja na kanisa hili la Ufufuo na Uzima Tawi la Iringa” walisema wananchi
Posted by MROKI On Tuesday, April 23, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo