Nafasi Ya Matangazo

March 07, 2019

Mtangazaji Mahiri wa Clouds FM, Ephrahim Kibonde (pichani juu) amefariki Dunia. 

 Taarifa za za kifo cha Kibonde zimeanza kusambaa asubuhi ya leo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza ,John Mongella amethibitisha kufariki kwa mtangazaji huyo kutokana na kusumbuliwa na presha.

Imeelezwa kuwa Kibonde alianza kusumbuliwa na Presha tangu akiwa Bukoba kwenye msiba wa Marehemu Ruge Mutahaba na baadae akahamishiwa Mwanza kwa uangalizi zaidi.

Aidha Mkuu wa vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga amethibitisha kufariki Dunia kwa Ephrahim Kibonde leo asubuhi katika hospitali ya Bugando,jijini Mwanza.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN.

TUTAENDELEA KUWALETEA TAARIFA ZAIDI ,KADIRI YA ZITAKAVYOKUWA ZINATUJIA
Posted by MROKI On Thursday, March 07, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo