Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania, Luhaga Mpina (wapili kushoto) ambaye ndiye Makamo Mwenyekiti wa Oganaizesheni ya Uvuvi wa Ziwa Victoria (LVFO), inayojumuisha nchi wanachama wa Afrika Mashariki akiangalia taarifa baada ya kutia saini ya makubaliano ya kuendesha Operesheni ya pamoja ya kudhibiti uvuvi haramu katika Ziwa Victoria mara baada ya kumaliza kuendesha kikao hicho jijini Arusha jana. Wengine kutoka Kushoto ni Waziri wa Kilimo,Wanyama na Uvuvi wa Uganda, Vincent Bamulangaki Ssempijja, Katibu Mkuu wa Uvuvi wa Kenya Prof. Micheni Ntiba aliyemwakilisha Waziri wake na Dkt.Deo-Guide Ruhema, Waziri wa Mazingira ,Kilimo na Mifugo wa Burundi. Picha na John Mapepele.
Mawaziri na Wawakilishi wa Mawaziri wanaosimamia Sekta ya Uvuvi wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakionyesha taarifa waliyotia saini ya makubaliano ya kuendesha Operesheni ya pamoja ya kudhibiti uvuvi haramu katika Ziwa Victoria mara baada ya kumaliza kikao hicho jijini Arusha.
Picha ya pamoja ya Watendaji, Makatibu Wakuu na Mawaziri wanaosimamia Sekta ya Uvuvi wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kumaliza kusaini makubaliano yao ya kuendesha Operesheni ya pamoja ya kudhibiti uvuvi haramu katika Ziwa Victoria. Picha na John Mapepel.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania, Mhe Luhaga Mpina ambaye ndiye Makamo Mwenyekiti wa Oganaizesheni ya Uvuvi wa Ziwa Victoria (LVFO), inayojumuisha nchi wanachama wa Afrika Mashariki na Mgeni wa Rasmi wa Mkutano huo akisoma hotuba yake kwenye mkutano wa (LVFO) jijini Arusha. Picha na John Mapepele.
**************
Na John Mapepele- Arusha
Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimetiliana saini makubaliano ya kuendesha Operesheni ya pamoja ya kudhibiti uvuvi haramu katika ziwa Victoria.
Makubaliano hayo ni mkakati wa nchi hizo za Kenya, Uganda na Tanzania, kulinda rasilimali hizo ziwe endelevu na zitumike kukuza uchumi wa wananchi wa mataifa hayo. Makubaliano hayo yamefikiwa katika Mkutano wa Mawaziri wa Sekta za uvuvi zinazozungukwa na Ziwa Victoria, uliofanyika Makao makuu ya Jumuiya ya Afrika mashariki Jijini Arusha, Tanzania.
Makamu Mwenyekiti wa Mawaziri wa Sekta za uvuvi wa Jumuiya hiyo, Mhehimiwa Luhaga Mpina, alisema uamuzi huo utawezesha kuongezeka kwa samaki na mazao yake katika Ziwa Victoria.
Alisema hatua itachochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa wananchi wanaozunguka ziwa hilo ikiwa ni pamoja na kuongeza kipato chao.
Alisema wananchi wa Afrika mashariki wanaozungukwa na ziwa Victoria walikuwa wanalazimika kuagiza samaki kutoka nchi ambazo hazina hata maziwa,licha ya ziwa hilo kuwa na uwezo wa kulisha bara la Afrika kama litatunzwa vizuri.
Alisema samaki wachanga waliokuwa ziwani chini ya sentimita 50 walikuwa asilimia 96.3lakini kutokana na jitihada zilizofanywa za kudhibiti uvuvi haramu vifaranga vimepungua hadi kufikia asilimia 62.8 kiwango ambacho kinakubalika kwa vifaranga kuwepo majini.
Pia alisema samaki wanaoruhusiwa kati ya sentimita 50 hadi 80 waliokuwa wamebaki majini walikuwa asilimia 3.3 lakini baada ya kazi ya mwaka mmoja wameongezeka hadi kufikia asilimia 32 huku wale wenye urefu wa kati ya sentimita 80 hadi 85 ambao ni samaki wazazi walifikia asilimia 0.4 lakini kwa sasa wameongezeka na kufikia asilimia 5.2 kiwango ambacho kunakubalika.
Alizipongeza Taasisi za utafiti za Kenya, Uganda na Tanzania kwa umakini na umahiri wa kukusanya taarifa za kitafiti ili kuzisaidia nchi wanachama kupanga yale ya usimamizi wa rasilimali za uvuvi.
“Tumefanya maamuzi makubwa ya kupanga mipango ya kufanya opersheni ya pamoja ili kuwa na uwelewa wa mpango ya pamoja ya namna ya kulitunza ziwa letu na kupambana na uvuvi haramu ya mazao ya uvuvi” alisema.
Nchi hizo zimekubaliana ziwe zimelipa madeni yote kkufikia juni, mwaka huu ilil kuwezesha Taasisi ya Uvuvi ziwa victoria (LVFO) kutekeleza mipango yake kwa wakati.
Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mtendaji wa Oganaizesheni ya Uvuvi wa Ziwa Victoria (LVFO) Dkt. Shigalla Mahongo alisisitiza kuwa na umoja katika kuhifadhi raslimali za uvuvi katika ziwa hilo kwa kuwa idadi ya watu katika nchi wanachama wa jumuiya ya Afika Mashariki ikekuwa ikikuwa kwa kasi na kuendelea kutegemea samaki wa ziwa hilo kwa kiasi kukubwa.
“Idadi ya watu ilikuwa milioni 23.5 mwaka 1954 wakati Sangara walipowekwa katika ziwa Victoria lakini mwaka 2018 inakadiriwa kuwa idadi ya watu iliongezeka kwa takribani mara 7 na kufikia jumla ya watu wapatao milioni 165.5 ambapo sasa inakadiriwa kufikia mwaka 2050 kuwa na zaidi ya watu milioni 323.1 hiyo ina maana kuwa itakuwa ni mara 14 ya idadi ya watu waliokuwa mwaka 1954 wakati ziwa likiwa bado ni lilelile” alionya Dkt. Mahongo.
0 comments:
Post a Comment