Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akizungumza na wananchi waliofika kwa ajili ya kuwasilisha kero juu ya Ardhi katika ukumbi wa mikutano wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) usharika wa Hai mjini.
Katibu tawala wa wilaya ya Hai,Upendo Wella akizungumza wakati wa siku ya kwanza iliyotengwa na Wilaya ya Hai kushughulikia kero zinazohusua masuala ya migogoro ya Ardhi katika wilaya hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akizungumza katika mkutano huo wa kushughulikia kero za Ardhi katika wilaya hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo (kushoto) akimueleza jambo mkuuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya (kulia) wakati wa siku ya kusikiliza kero juu ya masuala ya Ardhi inayofanyika katika mji wa Bomang'ombe.
Katibu tawala wa wilaya ya Hai,Upendo Wella akimueleza jambo mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya wakati wa usikilizaji wa keo juu ya masula ya ardhi katika wilaya ya Hai.
Baadhi ya wakuu wa idara katika Halmashauri ya wilaya ya Hai wakisiliza malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu masuala ya ardhi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akisikiliza malalamiko juu ya masuala ya Ardhi kutoka kwa wananchi wa wilaya hiyo.
Katibu tawala wilaya ya Hai,Upendo Wella akiwa na Mkaguzi wa Polisi,Inspekta Shabo wakichukua maelezo kutoka kwa mmoja wa wananchi walowasilisha malalamiko yao juu ya masuala ya Ardhi.
Mkuu wa wilaya ya Hai.Lengai Ole Sabaya akimsikiliza mmja wa wananchi waliojitokeza kutoa malalamiko yake juu ya suala la Ardhi .
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yoahana Sintoo wakitizama moja ya malalamiko makubwa ya Ardhi ktaika wilaya hiyo ,lalamiko linalowahusu watu zaidi ya 300 wa eneo la Gezauleole .
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya
Kaskazini.
SERIKALI katika wilaya ya Hai imetangaza kubatilisha
umiliki wa viwanja 34 kati 52 vilivyopo
kwenye eneo la maendelezo ya viwanda la Weruweru katika Wilaya ya Hai, mkoani
Kilimanjaro kutokana na madai mbalimbali ikiwemo kutoyaendeza.
Madai mengine ya
kuandikwa kwa ilani hiyo kwa Waziri wa Ardhi, , Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, imetajwa
kuwa ni wamiliki wa maeneo hayo ni deni
la fedha za Pango la Ardhi kwa zaidi ya miaka 20.
Wanaotajwa kumiliki
maeneo hayo wamo pia viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wa serikali
wastaafu,wafanyabiashara ,kampuni zinazo miliki mashamba makubwa pamoja na taasisi
zisizo za kiserikali.
Akizungumza katika
mkutano wa kwanza wa kushughulikia kero zinazohusu masuala ya Ardhi ,Mkuu wa
wilaya ya Hai ,Lengai Ole Sabaya amesema tayari Halmashauri imewasilisha barua
kwa Waziri wa Ardhi ili kumfikishia rais wa Jamhuri ya muungano Tanzania kwa
ajili ya utiaji saini.
Idadi hiyo ya watu 34, inafanya jumla ya kiasi
cha fedha kinachodaiwa kutokana na pango la ardhi kufikia Sh. 1, 828, 166, 096.
Waliotajwa katika orodha ya wamiliki wa viwanja
hivyo ni pamoja na Mbunge w jimbo la Hai, Freeman Mbowe ,Mkuu wa mkoa wa zamani
wa Kilimanjaro, Cynthia Hilda Ngoye, Kiwanda cha Kutengeneza Vipuri cha
Kilimanjaro Mashine Tools Manufacturing Company Ltd kilichopo chini ya Shirika
la Taifa la Maendeleo (NDC) na wafanyabiashara maarufu wa mji wa
Moshi na wamiliki wa shule binafsi na makampuni ya utalii.
Sabaya alisema watu hao wamo katika orodha ndefu
ya wamiliki ambao viwanja vyao vimeombewa kibali cha kufutwa na kwamba kwa
mujibu wa orodha hiyo, Kiwanda cha Mashine Tools kina deni la Sh. milioni
315,720,720 ambalo inadaiwa kati ya mwaka 2010 hadi 2018.
“Huko nyuma watu walipewa viwanja mashine tools,
viwanja 52 vikubwa wakaambiwa waendeleze kwa sababu ni eneo la viwanda, wana
miaka mingapi? Afisa Ardhi yuko wapi, njoo, nini kimetokea pale.
“Sasa sikilizeni huo mziki, unapewa shamba (eneo
la kiwanja) mwaka 1984, mmesikia? kabla mimi sijazaliwa, hajawahi kufanya
lolote, akapewa na halmashauri ili waendeleze kujenga viwanda. Sasa Afisa Ardhi
ameshaandika barua ya kubatilisha hivyo viwanja…Niwaambie hapa hapa wako watu
mnaowaheshimu na hawalipi kodi na leo ntawataja humu.”
Katika mkutano huo, Mkuu huyo wa Wilaya alipokea
malalamiko 266 yanayohusu ardhi na kuahidi ndani ya siku mbili yatakuwa
yamepata majibu.
Katika mkutano huo, Kaimu Kamishna wa Ardhi
Msaidizi wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Alphonce Lekule, aliwaeleza wananchi
wa Hai kwamba kuwapo idadi kubwa ya malalamiko ni kwa ni changamoto kwa watendaji
wa ardhi.
0 comments:
Post a Comment