VIONGOZI wa Vitongoji na Vijiji
vilivyopo kwenye mipaka mkoani Tanga wameonywa kuacha tabia ya kuuza
ardhi kwa wageni wanaofika kwenye maeneo yao badala yake hakikishe
wanatoa taarifa wanapowaona watu wasiowajua ili kuweza kukomesha vitendo
vya wahamiaji haramu.
Hayo yalisemwa na Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga Crispian Ngony’ani wakati
akizungumza na vyombo habari ambapo alisema viongozi hao wamekuwa ni
tatizo kubwa badala ya kukemea vitendo vya wahamiaji haramu lakini
wamekuwa wakiwakumbatia kwa kuwapatia ardhi jambo ambalo ni kosa
kisheria.
Alisema utafiti walioufanya mpakani mwa Kenya na Tanzania Horohoro
wamebaini idadi kubwa ya wakenywa wameuziwa ardhi katika maeneo hayo na
wanaishi nchini kinyume cha sheria huku akiwataka viongozi hao kuachana
na vitendo hivyo kabla hawajakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya
dola.
“Tatizo kubwa viongozi wa vitongoji na vijiji badala ya kumemea uuzaji
wa ardhi kinyemele hivyo napenda kutoa onyo kwao kuacha tabia hiyo kwani
sisi kama idara ya uhamiaji tupo macho kuhakikisha wale wote
wanaohusika na vitendo hivyo tunawachukulia hatua “Alisema.
Alisema viongozi hao badala ya kukemea uzaji wa haramu ardhi kwa wageni
wao wamekuwa mstari wa mbele kuwakarabisha kwenye maeneo hayo bila
kutambua kufanya hivyo ni makosa kisheria hivyo kuwaonya kuacha vitendo
vya namna hiyo mara moja.
“Pindi wanapomuona mgeni au raia anauza ardhi watoe taarifa kwenye
vyombo vinavyo husika ikiwemo idara ya uhamiaji tukishirikiana kwa
mtindi huo tutaweza kukomesha vitendo vya watu kuvamia ardhi yetu na
kuishi kinyume cha sheria tu “Alisema Ofisa Uhamiaji huyo.
Wakati huo huo,Ofisa Uhamiaji huo alisema katika kipindi cha mwaka 2017
wamekamatwa watanzania 61 kwa kuvunja sheria za uhamiaji ambapo kosa
kubwa ni kushiriki vitendo viovu vya kuwasafirisha wahamiaji hao katika
maeneo mbalimbali na kuwaingiza nchini.
Alisema hasa wahamiaji ambao ni raia kutoka nchini Ethiophia
wanaonekana wana biashara kubwa sana kwa baadhi ya watu mkoani Tanga kwa
kwenda nchini Kenya kuwachukua kwa kufanya udalali na kuwapitisha
kwenye njia za panya hadi kwenye maeneo wanayotaka kufika.
Aidha alisema kutokana na hali hiyo idara hiyo imeweka mikakati kabambe
ya kuhakikisha wanakomesha vitendo vya namna hiyo kwa kuongeza udhibiti
wa watu wanaoingia nchini kwa kushirikiana na vyombo vya vyengine vya
dola.
Hata hivyo alisema katika kipindi hicho kesi 28 zimefunguliwa ambazo
zilikuwa zinawahusu watanzania na zilizokuwa zikiendelea ni 10,nne
zilikwisha,mbili zilifutwa na moja iko kwa wakili wa serikali na
nyengine moja ipo uhamiaji.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya
Tanga Raha)
0 comments:
Post a Comment