Makamu Mwenyekiti TATO Henry
Kimambo katikati akifungua duka kubwa lavifaa mbalimbali vya mapishi kwenye
mahoteli linalomilikiwa na kampuni ya kimataifa ya PiMAK ambao ni watengenezaji
na wauzaji wa bidhaa hiyo ,Duka hilo lilifunguliwa juzi eneo la njiro jijini
Arusha,Kulia ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez ( Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
Makamu Mwenyekiti
TATO Henry Kimambo ambaye alikuwa mgeni rasmi akiingia katika duka kubwa lavifaa mbalimbali vya mapishi kwenye mahoteli linalomilikiwa na kampuni
ya kimataifa ya PiMAKambao ni watengenezaji na wauzaji wa bidhaa hizo ,Duka
hilo lilifunguliwa juzi eneo la njiro jijini Arusha,kulia ni Meya wa jiji la
Arusha Kalist Lazaro
Kulia ni Mbunge wa Arusha Godbless Lema
akiteta jambo na Mkurugenzi wa hoteli ya Gold Crest ya Mwanza na Arusha Mathias
Manga mara baada ya kuwasili katika ufunguzi wa duka kubwa lavifaa mbalimbali
vya mapishi kwenye mahoteli linalomilikiwa na kampuni ya kimataifa ya PiMAK
Meneja Mkuu wa kampuni ya PiMAK ya kimataifa
inayojihusisha na utengenezaji na uuzaji wa vifaa mbalimbali vya mapishai
kwenye mahoteli akitoa maelezo kwa mteja aliyetembelea duka hilo
Meneja Mkuu wa kampuni
hiyo, Ali Donmez akimuonyesha bidhaa za kampuni ya PiMAK mtaja aliyetembelea duka hilo siku ya uzinduzi Bi.Mary Mbajo
Wahudumu wa duka hilo wakiwa na
vepeperushi vya kampuni hiyo. BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.
Muonekano ndani ya duka hilo
Makamu Mwenyekiti TATO Henry Kimambo akizungumza mara baada ya kukata utepe,kushoto ni diwani wa kata ya Themi jijini Arusha ,Milance Kinabo
Naibu Meya wa jiji la Arusha,Viola
Likindikok akiangalia baadhi ya vyombo vinavyopatikana
dukani hapo anayefatia ni Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro
Kulia
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez akipozi na wadau katikati ni Maya wa jiji Kalist Lazaro
Mbunge wa Arusha Godbless Lema akiteta jambo na wadau wa kampuni hiyo
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez akitoa maelezo kwa mteja
Wageni
waliofika katika uzinduzi huo wakibadilishana mawazo
***************
Na Pamela Mollel,Arusha
KAMPUNI
ya kimataifa ya PiMAK inayojihusisha na
utengenezaji na uuzaji wa vifaa vya mbalimbali vya mapishi kwenye mahoteli , imefungua
duka kubwa jijini Arusha kwaajili ya kuwarahisishia watumiaji wa vyombo hivyo
kuvipata kwa wakati
Akizungumza
katika uzinduzi wa duka hilo la kisasa Makamu
Mwenyekiti TATO Henry Kimambo ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kuwepo kwa duka hilo hapa Tanzania tayari ni fursa kubwa kwa wafanyabiashara wa mahoteli
Kimambo alisema kuwa kampuni ya PiMAK kuja kuwekeza nchini
itasaidia ajira lakini pia kuwainua wajasiriamali wadogo wenye ndoto ya kufika
mbali
“Kuna hawa wajasiriamali wadogo ambao wanajihusisha na
maswala ya upishi watapata fursa ya kutanua biashara zao kwa kuwa tayari vifaa
vinapatikana kiurahisi”alisema Kimambo
Meneja
Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez alisema, kampuni hiyo yenye makao yake Uturuki
imeamua kufungua maduka hapa Nchini Tanzania kwaajili ya kuwarahisishia wateja
wake ambao walikuwa wakiagiza vyombo hivyo nje ya nchi
Akizungumzia
kuhusiana na bidhaa hizo, alisema kuwa ni bidhaa kwa ajili ya matumizi ya
hoteli, migahawa na huduma kubwa za mapishi vikiwamo vya kukatia nyama, kuhokea
mikate, kuoshea vyombo, kupikia na huduma nyingine za kihoteli
0 comments:
Post a Comment