Nafasi Ya Matangazo

August 23, 2017

WILAYA ya  Kibondo mkoani Kigoma, inayokadiriwa kuwa na wakaazi zaidi ya laki mbili, hadi sasa lakini  ni wananchi 60 tu ndio wanahati za kumiliki ardhi.

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Wilaya hiyo Louis Burra ameunda tume mbili zitakazo chunguza  idara ya  ardhi na kuchunguza masuala ya Migogoro ya ardhi na kwanini Wilaya hiyo ina hati chache ilikuhakikisha migogoro hiyo inakwisha na Wananchi wanapata hati. Anaandika Rhoda Ezekiel Kigoma.

Akizungumza jana katika kikao cha baraza la madiwani cha kufunga robo ya Mwaka,Mkuu wa Wilaya ya Kibondo  Bura alisema migogoro ya ardhi katika halmashauri hiyo imekuwa ikiongezeka kila siku, na haiwezekani mpaka sasa halmashauri ina hati 60 tuu na Wilaya inazaidi ya wakaazi laki mbili na viwanja havijapimwa.

Alisema atashirikiana na Mkurugenzi kuhakikisha anaunda tume ya uchunguzi itakayo fanya uchunguzi ni kitugani kinasababisha migogoro inaendelea na baada ya uchunguzi watahakikisha Wanawachukulia hatua za Kinidhamu watumishi wote wanaosababisha matatizo hayo.Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
"Suala la migogoro ya ardhi limekuwa kero kwa Wananchi wa Kibondo hatuwezi kuvumilia jambo hili sitakubali suala hili liendelee, tutaangalia kama kunarushwa inaendelea au kama kunaudanganyifu unaendelea tukibaini tutawashughulikia, na hati niwaombe watumishi kwa kushirikiana na Mkurugenzi muhakikishe mnapima viwanja na kuwapatia hati wananchi ilituweze kupata mapato kupitia kodi zitakazo tolewa na Wananchi", alisema Bura. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


Aidha Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Juma Mnwele, alisema changamoto inayo sababisha migogoro hiyo kuendelea kuwepo ni utendaji kazi wa mazoea wa Watumishi na Watumishi kutokuwa wabunifu kunasababisha hati kuwa chache na kuipotezea halmashauri hiyo kukosa mapato kutokana na kodi zinazotolewa na Wananchi kupitia viwanja vyao.

Alisema halmashauri hiyo imeandaa utaratibu wa kuanza kupima Viwanja katika eneo la Nengo ilikuweza kuwagawia Wananchi wote wenye migogoro, iliyotokana na wengi wao kujikuta wakigawiwa kiwanja kimoja kwa watu zaidi ya mmoja na wote wenye tatizo hilo watagawiwa viwanja bure, na upimaji huo utasaidia kuongeza upatikanaji wa hati na utaambatana na urasimishaji wa maeneo kwa Wananchi iliwaweze kupata hati.

Alisema lengo la halmashauri hiyo ilikuwa ni kutoa hati elfu nne mpaka sasa wamekwisha kutoa hati 40, ni kutokana na mji huo kuwa mkongwe na haukuwa umepangwa wala kupimwa, baada ya kupimwa anaamini hati zitaongezeka na Wananchi wstapata hati waweze kuombea mikopo na kufanyia mambo yao binafsi.

Kwa upande waje Mbunge wa Jimbo la Muhambwe, ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Maliasili na Ardhi, Atashasta Nditiye alisema mji wa kibondo watu wasio waaminifu wamekuwa wakigawa viwanja kwa watu zaidi ya mmoja ndio chanzo cha migogoro yote kakita Wilaya.

Hata hivyo Nditiye alieleza kuwa kamati yao wamepanga kupima maeneo yote i makusudi kwaajili ya shughuli maalumu , na kutenga maeneo kwaajili ya Wakulima, wafugaji, huduma za kujamii na makazi ilikuhakikisha migogoro yote inamalizika na Wananchi wanapata maeneo yao kwa uhalali.

"Kitu tunacho fanya ni  kupanga mji wa kibondo ili wananchi wasio na hati wapate,tumejipanga kuanza kupima viwanja kila kiwanja kitakachokuwa kikitolewa kwa  Wananchi kitakuwa kikipimwa na kugawiwa hati hapo hapo tumeandaa  wapima kwaajili ya kulasimisha makazi ya wananchi waweze kupata hati",alisema Nditiye.

 Alisema tatizo lililo changia mji wa kibondo kuwa na hati chache ni ulasimu kwa baadhi ya watendaji kuonyesha mlolongo mrefu wa upatikanaji wa hati, na wananchi hawakuona umuhimu wa kuwa na hati na kuwaomba Wananchi kufuata utaratibu na sheria kabla ya kununua viwanja ilikuepukana na udanyanyifu pamoja na migogoro.

 Keneddy Surungali ni Mwananchi wa Wilaya ya Kibondo,alisema idadi ya wasio na hati ni wengi, na kinacho wafanya Wananchi kushindwa kumiliki hati ni baadhi ya Watumishi kusahau na mkakati ulioweka na serikali wa hati hadi ikasainiwe na waziri inasababisha uchelewaji na gharama kubwa iliyo wekwa ili upate hatiunatakiwa utoe Kiasi cha shilingi lakimbili iliaweze kupata .

Posted by MROKI On Wednesday, August 23, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo