Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (Mb), wapili kulia, akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, kutembelea mradi wa umeme wa Kinyerezi II na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam, Agosti 21, 2018. Kamati hiyo pia ilitembelea kituo cha kupkea gesi asili kilicho jirani na Miradi hiyo.
Dkt. Kalemani (katikati mbele), akiwaongoza wajumbe hao baada ya kutembelea eneo la mradi wa upanuzi Kinyerezi I
Hili ndio eneo la upanuzi wa mradi wa umeme Kinyerezi II
Mtandao wa mabomba ya kusafirisha gesi asilia kutoka kituo cha kupokea gesi hiyo kuelekea eneo la miradi hiyo.
Mafundi wa TPDC wakiwa wamesimama kwenye eneo la utandazaji wa mabomba hayo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Hawa Ghasia, (wapili kushoto), akizungumza jambo wakati akiongozana na Naibu Waziri Dkt. Kalemani (kushoto) na wajumbe wa kamati.
Dkt. Kalemani akiongea wakati wa ziara hiyo.
Mhe. Hawa Ghasia akizungumza baada ya ziara ya kutembelea kituo cha kupokea gesi asilia kinachosimamiwa na TPDC.
Wajumbe wa Kamati wakipita pembezoni mwa moja ya mashine kubwa (genereta), kati ya 8 zinazofungwa kwenye mradi wa Kinyerezi II
Mhandisi Manda, (waliyenyoosha mkono), ambaye ni Meneja Mradi wa Kinyerezi II, akwapatia maelezo wajumbe wa Kamati akiwemo Naibu Waziri Dkt. Kalemani.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAMATI ya
Bunge ya Bajeti, imetembelea miradi ya kuzalisha umeme wa gesi ya Kinyerezi II,
na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I unaoendeshwa na Serikali kupitia Shrika la
Umeme Tanzania (TANESCO) na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo.
Kamati
hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Mtwara vijijini Mhe. Hawa Ghasia, pia
ilitembelea kituo cha kupokea gesi asili inayotumika kuzalisha umeme kilichoko
jirani na miradi hiyo.
Katika
ziara hiyo, mwenyeji wa Kamati hiyo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, (Mb),
Mhe.Dkt.Medard Kalemani, aliwahakikishia wajumbe wa Kamati hiyo kuwa miradi
hiyo inaendelea kama ambavyo Serikali ilitarajia na kwamba Watanzania wategemee
ongezeko kubwa la upatikanaji wa umeme pindi miradi hiyo itakapokamilika.
“Mhe. Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Kamati, miradi hii kunzia ule wa Kinyerezi I unaopanuliwa ambapo kutakuwa na ongezeko la umeme Megawati 35 na hivyo kufanya jumla ya Megawati 185 zitakazozalishwa kutoka Kinyerezi I, na huu wa Kinyerezi II utakapokamilika Agosti mwakani (2018) utatupatia Megawati 240 na ukijumlisha na miradi mingine itakayofuatia ya Kinyerezi III na VI, tutakuwa na jumla ya Megawati 1175.” Alifafanua Mhe. Dkt. Kalemani.
“Mhe. Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Kamati, miradi hii kunzia ule wa Kinyerezi I unaopanuliwa ambapo kutakuwa na ongezeko la umeme Megawati 35 na hivyo kufanya jumla ya Megawati 185 zitakazozalishwa kutoka Kinyerezi I, na huu wa Kinyerezi II utakapokamilika Agosti mwakani (2018) utatupatia Megawati 240 na ukijumlisha na miradi mingine itakayofuatia ya Kinyerezi III na VI, tutakuwa na jumla ya Megawati 1175.” Alifafanua Mhe. Dkt. Kalemani.
Kwa upande
wake Meneja wa Mradi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephene Manda aliwaambia
wajumbe wa kamati hiyo kuwa mradi huo utakuwa na jumla ya mashine 8 ambazo
zitafua umeme na tayari ufungaji wa mashine hizo umeanza na unaendelea na
kuongeza kuwa kuanzia Desemba Mosi mwaka huu, TANESCO itaingiza megawati 30
kwenye gridi ya taifa na kufanya hivyo kila baada ya mwezi mmoja kadri kazi ya
ufungaji wa mashine hizo utakavyokuwa unakamilika.
Alisema
gharama za mradi
wa Kinyerezi II ni dola milioni 344.
Wajumbe wa
Kamati hiyo pian walipata fursa yua kujionea kazi ya utandazaji wa mabomba
makubwa ya kupitisha gesi kutoka kituo cha kupkea gesi kuelekea kwenye eneo la
miradi hiyo.
“Niwapongeze
sana kwa kazi nzuri mnayoifanya na haya ndio matarajio ya wabunge kuona kuwa
miradi hii ambayo inagharimu fedha nyingi za walipa kodi inakamilika kwa wakati
ili hatimaye serikali iweze kutekeleza mipango yake ya ujenzi wa uchumi wa
viwanda kama ilivyoahidi wananchi.”Alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Bajeti, Mhe. Hawa Ghasia. Baada ya kumaliza ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi
hiyo ya umeme wa gesi asilia.
0 comments:
Post a Comment