Waziri wa Maliasilia na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka baina ya Hifadhi za Taifa, Wahiri na Waandishi wa aandamizi wa habari nchini, ulioanza leo jijini Tanga.Picha zote:Katuma Masamba.
**************
Wanahabari nchini wametakiwa kuhakikisha wanatumia kalamu zao vizuri katika kuandika masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya utalii nchini hatua itakayosaidia kukuza sekta hiyo na patobla taifa kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe wakati akifungua mkutano wa sita wa wahariri na wanahabari waandamizi unaohusu sekta ya utalii nchini ambao umeandaliwa na Hifadhi za Taifa (TANAPA) unaofanyika jijini Tanga.
Waziri Maghembe amesema sekta ya habari ina mchango mkubwa katika kukuza sekta ya utalii nchini, hivyo wanahabari wanatakiwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa jamii kupitia habari na makala mbalimbali wanazoandika.
"Mchango wa vyombo vya habari ni muhimu sana katika kukuza sekta ya utalii, mmekuwa mnaandika sana lakini naomba muendeleevkuandika zaidi ili tuweze kuwa na sekta ya utalii yenye ustawi mzuri," amesema.
Amesema kwa sasa watu mbalimbali duniani wanafahamu kuhusu vivutio vilivyopo nchini na hiyo ni kutokana na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi amesema wataendelea kushirikiana na vyombo vya habari ili kuhakikisha watanzania na watu mbalimbali duniani wanavifahamu vizuri vivutio vyvutalii vya Tanzania.
Meneja mahusiano wa shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) Pasco Shelutete akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo hii leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi akizngumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jijini Tanga leo.
Washiriki wa mkutano hao wakifuatilia hotuba za ufunguzi zilizokuwa zikitolewa na viongozi mbalimbali.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani, Dk James Wakibara akiwasilisha mada ya changamoto za mifugo katika hifadhi za taifa katika mkutano huo.
Maofisa wa TANAPA wakifuatilia mada
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano huo.
Picha ya pamoja baina ya washiriki na mgeni Rasmi.
0 comments:
Post a Comment