Meneja Uendeshaji wa
Multichoice Tanzania Baraka Shelukindo akikabidhi mashuka kwa Mlezi wa kituo
cha kulelea watoto yatima cha Al-Madinnah kilichopo Tandale jijini Dar es
Salaam Kuruthum Juma (wa pili kulia). Wa pili Kushoto ni Malkia wa Taarabu Hadija
Kopa na kulia ni Muigizaji maarufu wa tamthilia ya Huba Riyama Ali ambao ni
mabalozi maalum wa DStv. Hafla hiyo ilifanyika jana katika kituo hicho ambapo
vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mbili vikiwemo vyakula,
mashuka, vyombo na mitungi ya kuzimia moto vilikabidhiwa
Meneja Uendeshaji wa
Multichoice Tanzania Baraka Shelukindo akikabidhi King’amuzi cha DStv kwa Mlezi
wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madinnah kilichopo Tandale jijini Dar
es Salaam Kuruthum Juma (wa pili kulia). Wa pili Kushoto ni Malkia wa Taarabu Hadija
Kopa na kulia ni Muigizaji maarufu wa tamthilia ya Huba Riyama Ali ambao ni
mabalozi maalum wa DStv. Hafla hiyo ilifanyika jana katika kituo hicho ambapo
vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mbili vikiwemo vyakula,
mashuka, vyombo na mitungi ya kuzimia moto vilikabidhiwa
KAMPUNI ya Multichoice
Tanzania imetoa zawadi ya sikukuu ya Idi kwa kituo cha kulelea watoto yatima
cha Al-Madinnah kilichopo Tandale jijini Dar es Salaam. Msaada huo wa vyakula
na vifaa mbalimbali umekabidhiwa kwa kituo hicho na Meneja Operesheni wa
Multichoice Baraka Shelukindo katika hafla fupi iliyofanyika kituoni hapo ambayo
pia ilihudhuriwa na mabalozi kadhaa wa DStv akiwemo malkia wa taarab Khadija
Kopa na muigizaji maarufu wa filamu Riyama Alli.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi zawadi hizo, Shelukindo amesema kwa takriban miaka mitano mfululizo
Multichoice imekuwa ikikisaidia kituo hicho kwa mambo mbalimbali. Amesema wanafanya hivyo kwa kutambua kuwa
malezi ya watoto waishio katika mazingira magumu ni jukumu la kila mtu na kila
taasisi.
“Tunatambua kuwa jukumu la kuwalea watoto kama hawa ambao kwa sababu
moja ama nyingine wamejikuta katika mazingira magumu ni letu sote. Hawa ni
ndugu zetu, watoto wetu, na pia ni tegemeo kubwa kwa taifa letu, hivyo
kuwasaidia ni jukumu letu”
Amesema mbali na kwamba
Multichoice imekuwa ikikisaidia kituo hicho mara kwa mara kwa kuwapa vyakula na
mahitaji mengine, lakini pia waliamua kufadhili uanzishwaji wa mradi wa
ushonaji ambao unakisaidia kituo hicho katika kujiingizia kipato.
“Tunajua kuwa
chakula, malazi na mambo mengineyo ni muhimu kwa maisha ya kila siku ya vijana
wetu, lakini pia tuliona ni busara kuwawekea kamradi japo kadogo ambako
wataweza kujipatia kipato. Tumefurahi sana kuona mradi huu unaendelea na
tunaamini kuwa wataweza kuuendeleza na
kuukuza ili uwasaidia Zaidi.” Alisema Shelukindo.
Kwa upande wake Mkuu wa
kituo hicho Mama Kuruthum Juma ameishukuru Multichoice kwa msaada wao wa mara
kwa mara kwa miaka mingi sasa. Amesema kitendo cha Multichoice kukisaidia kitua
hicho kwa mambo mbalimbali hususan mradi wa ushonaji kumewasaidia sana katika
kujipatia kipata japo kusaidia gharama za uendeshaji kituo hicho ambazo ni
kubwa.
“Kwa kweli gharama za uendeshaji kituo ni kubwa sana na kama
mnavyofahamu watoto wanaolelewa hapa hawana uwezo na wengi wao hawana wazazi,
hivyo ni jukumu letu kuwalea, kuwapa matibabu, na pia kuwasomesha, hili kwa
kweli ni jukumu kubwa na tunahitaji msaada kutoka kwa wadau mbalimbali” alisema
Mama Kuruthum
Amesema idadi ya watoto
imekuwa ikiongezeka lakini kituo hakina uwezo mkubwa kutokana na ufinyu wa eneo
na bajeti hivyo akawaomba wadau wengine kuangalia uwezekano wa kukisaidia kituo
hicho ili kiweze kuhudumia watoto wengi Zaidi.
Naye Malkia wa Taarabu –
Khadija Kopa amesema amefarijika sana kuona Multichoice inawajali watoto
hususan wale waishio katika mazingira magumu ambao aghalabu husahaulika na
jamii.
“Kwakweli Multichoice wamefanya jambo la maana sana. Ni vyema
tukaunganisha nguvu zetu kuwalea hawa watoto wetu kwani nao wana haki kama
watoto wengine” alisema Kopa.
Naye muigizaji Riyama
Ali amepongeza jitihada zinazofanywa na Multichoice pamoja na uongozi wa kituo
cha Almadinna katika kuwasaidia watoto hao. “Watoto hawa ni hazina ya taifa.
Tukiwasaidia hawa wakakua vizuri, wakapata elimu nzuri, kesho na keshokutwa
tutapata wabunge humu, mawaziri, wakurugenzi, wanamichezo, wasanii na
kadhalika. Tushirikian kuwale na hili ni jukumu letu sote na ni kitu
kinacholeta Baraka” alisema Riyama.
Kituo cha Al-Madinnah
Orphanage Centre kilianzishwa mwaka 2004na kwa hivi sasa kituo hicho
kinahudumia jumla ya watoto 65 ambapo 40 kati yao ni wavulana na 25 wasichana
na wengi wao ni wanafunzi wa shule za msingi.
0 comments:
Post a Comment