Kiongozi wa Wabunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Dar es Salaam, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela kairuki, akizungumza na Wanachama wa CCM na Viongozi wa UWT, wakati wa ziara ya wabunge hao katika Jimbo la Segerea Wilaya ya Ilala kuhamasisha wanachama kuhusu uchaguzi wa Jumuiya hiyo na Uhai wa Chama katika mkutano uliofanyika leo mchana kwenye Ukumbi wa CCM Liwiti Tabata Dar es Salaam.
Kiongozi wa Wabunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Dar es Salaam, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela kairuki, akizungumza na Wanachama wa CCM na Viongozi wa UWT, wakati wa ziara ya wabunge hao katika Jimbo la Segerea Wilaya ya Ilala kuhamasisha wanachama kuhusu uchaguzi wa Jumuiya hiyo na Uhai wa Chama katika mkutano uliofanyika leo mchana kwenye Ukumbi wa CCM Liwiti Tabata Dar es Salaam. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO) BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Wanachama wakifurahia na kushangilia
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonah Kaluwa, akizungumza kutoa baadhi ya kero za wapiga kura wake mbele ya mgeni rasmi Kiongozi wa Wabunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Dar es Salaam, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela kairuki, wakati wa ziara ya wabunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dar es Salaam, katika Jimbo la Segerea Wilaya ya Ilala kuhamasisha wanachama kuhusu uchaguzi wa UWT na Uhai wa Chama katika mkutano uliofanyika leo mchana kwenye Ukumbi wa CCM Liwiti Tabata Dar es Salaam.
Mgeni rasmi akiwasalimia wanachama wa ccm jimbo la Segerea wakati akiwasili ukumbini hapo
Baadhi ya Wanachama wa CCM Kata ya Kitunda wakimsikiliza kwa makini Kiongozi wa Wabunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Dar es Salaam, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela kairuki, wakati akiwahutubia katika mkutano wa kuhamasisha uchaguzi na kuimarisha chama kuelekea uchagzi wa UWT.
Kiongozi wa Wabunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Dar es Salaam, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela kairuki, akizungumza jambo na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar esSalaam, Janeth MAsaburi, wakati wa ziara ya wabunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dar es Salaam, katika Jimbo la Segerea Wilaya ya Ilala kuhamasisha wanachama kuhusu uchaguzi wa Jumuiya hiyo na Uhai wa Chama katika mkutano uliofanyika leo mchana kwenye Ukumbi wa CCM Liwiti Tabata Dar es Salaam.
Kiongozi wa Wabunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Dar es Salaam, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela kairuki, akiagana na baadhi ya wanachama wa CCM baada ya kumaliza kuwahutubia katika mkutano wa kuhamasisha wanachama kuhusu uchaguzi wa UWT na Uhai wa Chama katika mkutano uliofanyika leo mchana kwenye Ukumbi wa Kitunda CCM uliopo Kitunda jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Masaburi, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza, wakati wa ziara ya wabunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dar es Salaam, katika Jimbo la Segerea Wilaya ya Ilala kuhamasisha wanachama kuhusu uchaguzi wa Jumuiya hiyo na Uhai wa Chama katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa CCM Liwiti Tabata Dar es Salaam.
Wanachama wa CCM wakifurahia na kucheza kwa pamoja wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya Vioongozi wa meza Kuu.
*************
*************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam,
kimesema kitapambana kufa na kupona kuhakikisha majimbo sita yaliyochukuliwa na
upinzani yanarudi mikononi mwa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.
Aidha wabunge hao wamewataka viongozi waUmoja wa
Wanawake CCM (UWT) waliopoteza majimbo kutopewa tena nafasi katika chaguzi
zinazoendelea kwa maslahi ya uhai wa Chama.
Alisema ni muhimu kila mmoja kabla ya kuwania
nafasi ya uongozi ndani ya UWT kujipima na kujitafakari uwezo wake kama ana
kifua cha kukihakikishia chama kinarejesha majimbo hayo.
Akizungumza jana Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki akiongoza
ziara ya wabunge hao wilaya ya Kinondoni alisema hakuna haja ya kumuonea mtu
haya lengo ni kuhakikisha majimbo hayo yanarudi.
‘’Tutahakikisha CCM Mkoa wa Dar es Salaam
tunapambana kufa na kupona kurudisha majimbo sita yaliyochukuliwa na upinzani
yanarudi mikononi mwetu hakuna muda wa kusubiri tukikosea katika chaguzi za
ndani tumekosea baadae kushawishi na kurejesha uhai wa chama,’’alisema.
Alisema ni lazima kuingia katika chaguzi hizo
kwa kujitafakari na kutochukua fomu kwa waliosababisha kupoteza majimbo hayo
kutokana na kutojipanga kwao.
Angellah alisema ni jambo la ajabu na aibu
wanawake kukubali kupoteza majimbo hayo kwa kushindwa kujipanga na
kuhamasishana kujiandikisha kupiga kura.
Alisema wakati wa kujutia makosa ni sasa hivyo
Jumuiya hiyo ikiwa inaendelea na chaguzi zake ni muhimu wanachama wahakikishe
hakuna kuchaguana maswahiba ‘maboya’ na badala yake wachague mtu kwa sifa yake
ili aweze kuchapa kazi kwa umakini zaidi.
Alisema Kinondoni idadi ya watu waliochukua fomu
ukilinganisha na wanachama waliopo ni ndogo hali inayotishia kuwapo na hujuma
hivyo ni lazima kujipanga lengo si kuwa kiongozi kwa mazoea kwakuwa chama si
mali ya mtu mmoja.
‘’Ni aibu haiwezekani nafasi moja mtu mmoja au
wawili na yupo yeye na swahiba yake au boya lake haiwezekani ni lazima kuwa
makini hayo maboya mliyoweka yanaweza kuja kuibuka na matokeo yake chama
kikakosa nguvu ya kupambana kurejesha majimbo hayo,’’alisema.
Alisema kutokana na hali hiyo utendaji hautakuwa
na sifa stahiki bali utakuwa wa kuogopana na hakutakuwa wa kumkanya mwenzake.
Angellah alisema baada ya uchaguzi huo anaamini
kuwa makundi hayatakosekana lakini ni vyema kubaki na mtu ambaye ameshinda na
wote kumuunga mkono.
Pia alishitushwa na idadi ndogo ya vijana ambao
wanaingia katika chaguzi hizo huku akiwataka wasinyimwe nafasi kwa maana vijana
ndio taifa la leo na kesho.
Waziri Kairuki pia alibainisha kuwapo na harufu
ya ufisadi katika kata ya Ndugumbi Wilaya ya Kinondoni kutokana na matumizi
mabaya ya mali za UWT zikiwemo fedha na vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya
wanawake kujitafutia kipato.
Alisema hayo yamesababishwa na kutokuwa na
viongozi madhubuti wa kusimamia mali za chama.
‘’Tulipochaguliwa tulirudi kuwashukuru na
tulitoa mashine tatu za kusaga na tatu za kukoboa, Vyerahani Saba lakini huu ni
mwaka wa sita vinaozea Wilayani na vingine mtu kajimilikisha anatumia kama vya
kwake binafsi ni lazima sasa kuanza kufuatilia mali za UWT na kurejesha kwa
wanachama,’’alisema.
Aliongeza mbali na vifaa hivyo pia zilitolewa
mashine za kutotoreshea vifaranga na fedha za kodi kwa kila jimbo ni lazima
zirudi na kuelekezwa kwenye matumizi yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Katibu wa UWT Mkoa wa Dar es
Salaam Fatuma Maliyaga aliwataka wanachama wa Jumuiya hiyo kuachana na dhana
potofu wanaposhindwa chaguzi kwa kuwa na makundi na badala yake washirikiane
kwa maslahi ya Chama.
Alisema ipo haja ya kukubali mabadiliko kwa kuwa wakati huu watakaokiuka maadili
hawatakuwa salama.
0 comments:
Post a Comment