Kocha Mchezaji wa Timu ya Viongozi wa Mkoa wa Mbeya na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla akifundisha kwa kutumia chati maalum ya kufundishia kwa wachezahi wake.
Kocha Mchezaji wa Timu ya Viongozi wa Mkoa wa Mbeya na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla akitoa maelezo kwa wachezahi wake.
Kocha Mchezaji wa Timu ya Viongozi wa Mkoa wa Mbeya na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla akitoa maelezo kwa wachezahi wake.
KIKOSI cha timu ya mpira wa miguu cha mkoa wa Mbeya kibachojinoa kwa mchezo dhidi ya viongozi wa dini leo kimefanya mazoezi yake ya mwisho kabla ya mchezo utakaofanyika kesho katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.
Chini ya Kocha Mchezaji wa timu hiyo ambaye pia ndie Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, timu hiyo ilifanya mazoezi katika uwanja wa Magereza jijini Mbeya.
Akizungumza baada ya mazoezi hayo, Makalla alisema timu yake imejipanga vyema kulipiza kisasi katika mchezo huo ambapo mshindi atakabidhiwa Kombe la Amani 2017.
Makalla pia amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika dimba la Sokoine kushuhudia mpambano huo wa ainayake utakao kutanisha viongozi wa mkoa wa Mbeya na Viongozi wa Dini.
"Mechi ni kesho saa 10 :00 jioni uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya na Kiingilio ni bure,"alisema Makalla.
0 comments:
Post a Comment