Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (wapili kushoto) akishiriki kufanya usafi katika Soko jipya la Machinga lililoo nanenae jijini Mbeya leo.
Wananchi wakishiriki kufanya usafi.
Wafanyakazi wa Benki ya Akiba wakiwa na Mkoo wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla baada ya kufanya usafi.
Baadhi ya maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama walioshiriki katika kufanya usafi leo
MKUU
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amewaongoza wakazi wa jiji la Mbeya kufanya
usafi katika soko la wamachinga la Nanenane jijini humno leo.
Akizungumza
wakati wa kufanya usafi Makalla amewahimiza wakazi wa Mbeya kuunga mkono
kampeni ya kuliweka jiji la Mbeya na mkoa na halmashauri zote kuwa safi.
Aidha
Makalla ameishukuru Benki ya Akiba kutoa msaada wa Vifaa vya usafi, na wafanyakazi
wa Akiba Bank kushiriki kufanya usafi na Benki hiyo kukubali ombi lake kutoa mikopo kwa wamachinga.
Meneja
wa Akiba Tawi la Mbeya Amehaidi kukutana na wamachinga hao na wengine katika masoko
maalum kwanza kuwapa Mafunzo na baadaye kuwapatia mikopo.
Mbali
na Mkuu wa Mkoa na Wafanyakazi hao wa Benki pia viongozi wa vyama vya Siasa ,
vyombo vya ulinzi na usalama na wamachinga walijitokeza kufanya usafi katika soko
la nanenane ambalo litakalofunguliwa hivi karibuni kwa ajili ya Machinga
wapatao 1,500
Wakizungumza
katika risala yao wamachinga wamemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwasaidia kujengwa
kwa choo cha kisasa , kuwekwa umeme na Maji katika soko hilo na kuahidi kuhamia
sokoni hapo ifikapo Julai mosi.
Mkuu
wa Mkoa amemwagiza Mkuu wa usalama barabarani na Sumatra kuweka kituo cha
Daladala katika eneo hilo mapema wiki ijayo jambo ambalo wamachinga
wamelipongeza kwani litachochea biashara
0 comments:
Post a Comment