Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza katika mkutano wake wa kupokea kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi kwa utaratibu maalum aliyojiwekea kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya William Ntinika.
wananchi wakiuliza maswali
Wakazi wa jiji la mbeya waliohudhuria mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akifafanua jambo kwa wanahabari.
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amemeuagiza uongozi wa Wilaya, Jiji la Mbeya,Polisi, Sumatrapamoja na viongozi wa Bajaji, Daladala na Bodaboda kukutana na kuboresha namna ya utoajibhuduma ambao utaepusha ajali, msongamano katika jiji hilo.
Makalla amesema lazima jiji la Mbeya liwe safi na liwe la mfano katika kila nyanya ikiwepo ya utoaji huduma ya usafiri kulinganisha na maemeo mengine nchini.
Ameomba ushirikiano kwa viongozi, watendaji na wananchi kuunga Mkono jitihada hizo.
Katika kuhakikisha hilo linafanyiwa kazi haraka, Makalla ameahidi kuitisha mkutano muda wowote na wenyeviti na makatibu wa Mabaraza ya Ardhi ngazi ya Wilaya kufuatia malalamiko mengi kuelekezwa kwenye Mabaraza ya ardhi.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wa kusikiliza kero za wananchi utaratibu ambao ameuweka tangu alipoteuliwa mwezi machi mwaka jana ambapo Mkuu wa Mkoa husikiliza kero za wananchi mara mbili kwa mwezi.
Utaratibu huu umepongezwa na wananchi na umesaidia sana kutatua kero nyingi za wananchi.
0 comments:
Post a Comment