Nafasi Ya Matangazo

April 27, 2017

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lolangulu iliyopo kijiji cha Mbola mkoani Tabora wakisoma kwa kupitia njia ya mtandao baada ya Airtel kwa kushirikiana na Erickson pamoja  na taasisi  ya Earth iliyoko nchini Marekani  kuwawezesha wanafunzi hao kupata nyenzo za masomo kupitia mtandao kwa kupitia mpango ujulikanao kama “Studi Academy”
************
KATIKA kutimiza dhamira ya kutumia teknologia ya mawasiliano katika kuendeleza jamii kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na taasisi ya Earth iliyoko nchini Marekani imeanzisha mpango utakaowawezesha wanafunzi wa sekondari kupata nyenzo za masomo kupitia mtandao wao wa intaneti

Mafunzo hayo kwa kupitia mtandao yanayojulikana kama“Studi Academy” yanapatikana kupitia mtandao wa Airtel wa 3G. ambapo katika kijiji cha Mbola Mkoani Tabora Airtel kwa kushirikiana na Erickson wameboresha zaidi mawasiliano ya intaneti ya kasi ya 3G ili kuhakikisha kuwa shule na vituo vyahuduma za afya zinafaidika na mpango huu kabambe kwa kuinua upatikanaji wa huduma za masomo kupitia mtandao na kuanza kuwafaidisha wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lolangulu.


Akiongelea ujio na mafanikio ya mradi huo Mwalimu mkuu wa shule ya sekodari ya Lolangulu , Cleophas Bugomba alisema” Shule yetu imekuwa na changamoto ya walimu wa kutosha kwa masomo ya sayansi hivyo kuwepo kwa masomo haya kupitia mtandao kumesaidia kupunguza changamoto hii
kwa kiasi kikubwa.

Mafanikio haya tumeyaona kupitia matokeo ya mitihani ya kitaifa ya kidato cha pili ambapo ufaulu wa wanafunzi hususani katika masomo ya sayansi ikiwemo hesabu na fizikia umekuwa wa kiwango kikubwa pamoja nakuwepo kwa changamoto hizi za walimu wakutosha wa masomo hayo”.

Kwa upande wake mwanafunzi wa kitado cha tatu mwaka 2017 Irene Tamson ambayo pia ni mwanafunzi bora wa kike aliyefanya vizuri katika masomo ya sayansi kwa mkoa wa Tabora alisema” mpango huu wa “Studi Academy” unaowezeshwa na intaneti ya Airtel umenisaidia sana kufanya maswali mbalimbali na kupata majibu sahihi hapo hapo, kujifunza vitu vipya na kupata nyezo muhimu pindi nikijisomea binafsi au kwa makundi.

Tunafurahi kuweza kunganishwa na mtandao na kujifunza kutoka kwa wengine kutoka nchi za ulaya lakini pia kupata nyenzo muhimu za kujifunzia kwanjia ya technologia ya kisasa.”

Nae Meneja wa huduma kwa Jamii wa Airtel , Bi Hawa Bayumi alisema,“tunajisikia fahari kuwa na mtandao bora unaotuwezesha kutoa huduma kwa jamii ikiwemo mpango huu wa Studi Academy, lengo letu Airtel ni kutoa suluhisho kupitia teknolojia ya mtandao ili kuwafikia watanzania wengi zaidi ili wapate mafunzo kwa njia ya mtandao hasa kwa maeneo ya pembezoni”.


Mipango na dhamira yetu Airtel ni kuendelea kushirikiana na wadau wetu kama Ericsson na Health kutumia fursa ya mawasiliano kuiwezesha jamii kwa kurahisisha baadhi ya changamoto za elimu na afya,”. Alieleza Bi Bayumi

Airtel Tanzania pia kupitia mpango wake wa kuendelea kutoa mawasiliano  bora kwa kuzingatia ubunifu mwaka jana ( 2016) walishirikiana na VETA na kuzindua Applikesheni kabambe ya VSOMO ili kuwawezesha watanzania nchini kote kujisomea kozi za ufundi stadi kutoka kwenye vyuo vya Ufundi VETA kupitia simu za mkononi ili kutoa fursa kwa watanzania nchini kujiendeleza kielimu bila kujali changamoto zinazosababishwa na mazingira au ukosefu wa vifaa vyakujisomea karibu nao.

Posted by MROKI On Thursday, April 27, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo