Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa
Mgwatu ( kushoto) akizungumza na Meneja wa TEMESA Kigoma Mhandisi Hassan
Karonda (kulia) alipotembelea kituoni hapo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa
Mgwatu( mwenye shati la rangi ya bluu) akijadili jambo na mafundi wa karakana
ya TEMESA Kigoma alipotembelea kituoni hapo kujionea utendaji kazi.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. MussaMgwatu (aliyeketi)
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalam James Frank jinsi mfumo wa kielektroniki
wa kukatishia tiketi katika kivuko cha Ilagala Mkoani Kigoma unavyofanya kazi.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa
Mgwatu (wa pili kulia) akiongozana na
Meneja wa TEMESA Kigoma Mhandisi Hassan Karonda (kulia) baada ya kukagua kivuko
cha MV. Malagarasi kinachotoa huduma ya usafiri katika Mto Malagarasi kati ya
Ilagala na Kajeje mkoani Kigoma.
****************
Picha/habari na Theresia Mwami TEMESA kigoma
Shirika la umeme Tanzania TANESCO linadaiwa na Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA) Kigoma kiasi cha shilingi milioni 41 ikiwa ni
malimbikizo ya madeni kutokana na matengenezo ya magari mbalimbali yaliyofanywa
na shirika hilo mkoani humo.
Hayo yameelezwa na Meneja wa TEMESA Mkoa wa Kigoma Mhandisi
Hassan Karonda alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa Mtendaji Mkuu wa
TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu alipotembelea kituoni hapo.
Meneja huyo ameeleza kuwa kwa sasa TEMESA Kigoma ipo kaytika
operesheni ya kukusanya madeni kutoka kwa Taasisi na makampuni wanayoyadai.
“Mtendaji Mkuu
tunazidai Taasisi mablimbali kiwemo Shirika la Umeme Tanzania TANESCO shilling
million 41 mpaka sasa” alisema Mhandisi Karonda.
Hata hivyo Dkt. Mgwatu alimtaka Mhandisi Karonda kuhakikisha
kuwa anakusanya madeni yote anayodai
mkoani humo haraka iwezekanavyo.
“ Fuatilia ofisi kwa
ofisi kukusanya madeni ili kukiwezesha kituo hiki kufanya kazi zake kwa ufanisi
mkubwa” alisisitiza Dkt. Mgwatu.
Akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo Dkt. Mgwatu pia
alipata fursa ya kutembelea kivuko cha
MV. Malagarasi na kuona utendaji kazi wake.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt Mussa
Mgwatu yupo katika ziara ya kutembelea vituo vya TEMESA nchi nzima kujionea
utendaji kazi wa vituo hivyo.
0 comments:
Post a Comment