Rais John Magufuli akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari na wahariri wakati wa mkutano wake wa kwanza kufanya mahojiano na waanahabari tangu aingie madarakani Novemba 5,2015. Mahojiano haypo maalum na ya aina yake yalifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais John Magufuli akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari na
wahariri wakati wa mkutano wake wa kwanza kufanya mahojiano na
waanahabari tangu aingie madarakani Novemba 5,2015. Mahojiano haypo
maalum na ya aina yake yalifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Wahariri wa vyombo vya habari wakifuatilia kwa makini mahojiano hayo.
Bloggers ni miongoni mwa wanahabari waliopata fursa hiyo ya kushiriki katika mkutano huo.
Rais Dk John Pombe Magufuli leo Novemba 4, 2016 kwa
mara ya kwanza tangu aingie madarakani mwaka mmoja uliopita, amefanya mahojiano
na Wahariri na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na
nje ya nchi katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mahojiano hayo
yaliyorushwa moja kwa moja (Live) kupitia vyombo vya habari vya
Redio, Televisheni na Mitandao yamechukua muda wa saa 2 na dakika 40 ambapo
Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kujibu maswali yote yaliyoulizwa na wahariri
na waandishi wa habari na ambayo yalilenga kujua utendaji kazi wa Serikali ya
awamu ya tano katika kipindi cha mwaka mmoja tangu iingie madarakani.
Katika majibu yake
Rais Magufuli amesema katika kipindi cha mwaka mmoja Serikali yake imehakikisha
nchi inaendelea kuwa na amani, utulivu na umoja na pia imechukua hatua madhubuti
za kuchochea kasi ya maendeleo zikiwemo kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka
Shilingi Bilioni 800 hadi kufikia wastani wa Shilingi Trilioni 1.2, Kununua
ndege kwa ajili ya kurahisisha usafiri na kukuza sekta ya utalii, kuongeza
bajeti ya maendeleo katika bajeti ya Serikali kutoka asilimia 26 hadi kufikia
asilimia 40 na kujenga miundombinu ya barabara na madaraja.
Dkt. Magufuli
amezielezea hatua nyingine kuwa ni kulipa madeni ya ndani na nje ya nchi,
kuongeza mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu, kuongeza fedha za kununulia dawa na
chanjo, kubana matumizi kwa kuelekeza fedha nyingi katika utatuzi wa kero za
wananchi na kuimarisha uhusiano na ushirikiana na nchi mbalimbali duniani kwa
lengo la kuvutia uwekezaji katika viwanda, utalii, miundombinu na huduma za kijamii.
Aidha, ameongeza
kuwa Serikali imeweza kutoa fedha za ruzuku kwa shule za msingi na sekondari
kiasi cha shilingi Bilioni 18.77 kila Mwezi kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa
elimu bila malipo, imetoa fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 148 kwa ajili ya upanuzi
wa mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi I na uanzishaji wa mradi wa umeme wa
Kinyerezi II.
Kufuatia hatua
hizo na nyingine nyingi, Rais Magufuli amesema katika mwaka mmoja wa uongozi
wake nchi imeshuhudia ukuaji mzuri wa uchumi wa wastani wa asilimia 7.9 katika
robo ya pili ikilinganishwa na asilimia 7 ya mwaka jana na kupunguza mfumuko wa
bei kutoka zaidi ya asilimia 7 hadi kufikia asilimia 4.5 hivi sasa.
Dkt. Magufuli
amesema amedhamiria kuhakikisha Serikali inarekebisha kasoro zilizokuwa zikisababisha
upotevu wa mali ya umma, vitendo vya ulaji rushwa na uhujumu uchumi, matumizi
mabaya ya madaraka na kuijenga Tanzania mpya ambayo kila Mtanzania atanufaika
na rasilimali za nchi yake.
Rais Magufuli
ametoa wito kwa vyombo vya habari kufanya kazi zake kwa kutanguliza uzalendo,
kuepuka kutumiwa na watu wenye nia ya kutetea maslai yao binafsi, kuepuka
kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na
Serikali kurekebisha kasoro zilizokuwa zikisababisha nchi kwenda vibaya.
Dkt. Magufuli
amewapongeza Wahariri na Waandishi wa Habari kwa kazi kubwa wanayoifanya na
amewaahidi kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana nao ili kuhakikisha
wananchi wanapata taarifa sahihi kuhusu utendaji kazi wa Serikali na maendeleo
ya nchi yao.
0 comments:
Post a Comment